Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akimsikiliza kwa
makini Afisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama ya nchini Marekani,
Emmanuel Nwankwo (wapili kushoto) katika mkutano wao uliofanyika jijini
Washington DC katika Ukumbi wa Mkutano wa Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani. Katika mazungumzo yao maafisa hao wa Marekani wanatarajia
kutua nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji,
Polisi na Maafisa Forodha ya kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa
ajili ya kudhibiti mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikwemo silaha, dawa
za kulevya pamoja na bidhaa mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi
ambazo zinaweza kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi mbalimbali duniani.
Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa
Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani hata hivyo alipata
muda wa kuzungumza na maafisa hao baada ya kumuomba kukutana naye.
Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata
Mulamula. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wanne kushoto), Balozi wa
Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (watatu kushoto),
na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New
York, nchini Marekani, Tuvako Manongi wakiwa katika picha ya pamoja na
Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani pamoja na Maafisa wa
Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama ya nchini Marekani. Waziri Chikawe
alikutana na Maafisa hao wa Marekani, jijini Washington DC kujadiliana
masuala mbalimbali likiwemo la Maafisa hao wakitarajia kuja nchini
Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji, Polisi na
Maafisa Forodha ya kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa ajili ya
kudhibiti mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikwemo silaha, dawa za
kulevya pamoja na bidhaa mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi
ambazo zinaweza kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi mbalimbali duniani.
Waziri Chikawe yupo jijini Washington DC katika Mkutano wa Kimataifa wa
Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, hata hivyo alipata muda wa
kuzungumza na maafisa hao baada ya kuomba kukutana naye. Katikati ni
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment