Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akizungumza na binti wa miaka 19 ambaye ni mlemavu wa ngozi na
kutosikia, Masalu Masuka ambaye anaishi katika kituo cha watoto walemavu
cha Buhangija baada ya kukimbia kwao Bariadi kukwepa wauaji wa albino.
Binti huyo alijifungua mtoto wake akiwa kituoni hapo bila msaada wa
muuguzi.
MRATIBU
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, na Mkurugenzi mkazi wa Shirika
la Maendeleo la umoja huo (UNDP), Alvaro Rodriguez amehimiza serikali
kuchukua hatua zaidi kukabili mauaji ya watu wenye albinism.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari leo kufuatia taarifa ya kutekwa na
kuuawa kwa binti mwenye albinism wa umri wa mwaka mmoja, Yohana Bahati,
alisema pamoja na juhudi zilizopo sasa za kukabili mauaji dhidi ya watu
wenye albinism lazima ziongezwe.
Maiti ya
Yohana Bahati (1) aliyetekwa Februri 15 mwaka huu imekutwa katika kijiji
cha Shilabela Mapinduzi , kilomita chache kutoka nyumbani kwao Ilelema.
Mwili huo
umekutwa na polisi katika hifadhi ya Biharamulo jana Februari 17, 2015
majira ya saa 9 alasiri huku ikiwa imenyofolewa miguu na mikono. Mama
yake, Ester Jonas (30) bado hoi hospitalini Bugando akitibiwa majeraha
yaliyotokana na mapanga wakati akijaribu kumuokoa mtoto wake.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa
amembeba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Ghoke Maliwa anayelelewa kwenye
kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara
ya kukitembelea kituo hicho hivi karibuni mkoani humo.
Aidha
dada yake Tabu bahati (3) bado yuko katika ulinzi wa polisi wakati dada
yao mkubwa Shida Bahati (12) akiwa kwa ndugu zake kijiji kingine.
Alisema katika taarifa yake kwamba katika kipindi cha miezi miwili
Tanzania imeshuhudia kutekwa nyara kwa watoto wawili katika kanda ya
ziwa. Desemba mwaka jana mtoto Pendo alitekwa na kusababisha kizaazaa
kikubwa lakini pamoja na juhudi za kumtafuta mtoto huyo mpaka leo
hajulikani alipo.
Taarifa
hiyo imesema kwamba Umoja wa Mataifa unasikitishwa na vitendo hivyo vya
kikatili dhidi ya watoto hao wawili. Mashambulio dhidi ya watu wenye
albinism yanaelezwa kuwa yanasababishwa na imani za kishirikina na
kwamba kutoka mwaka 2000 hadi sasa watu wenye albinism 74 wameshauawa.
"
Mashambulizi haya yanaambatana na ukatili mkubwa, na wakati serikali
inafanya kila juhudi kukabili tatizo hili, juhudi kubwa zinastahili
kufanywa ili kukomesha mauaji na kulinda kundi hilo dogo la watu ambao
wako katika hatari kubwa " inasema sehemu ya taarifa hiyo.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma
ujumbe unaosema "DREAM BIG" kwenye T-shirt ya mtoto Agnes Kabika mwenye
ulemavu wa ngozi anayelelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi
alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho hivi karibuni.
Umoja wa
Mataifa umesema kwamba mashambulio dhidi ya albino hayavumiliki, si
halali kwa namna yoyote na yanaweza kukomeshwa. Wakati taifa hili
linaelekea katika uchaguzi, yapo madai kuwa maisha ya watu wenye
albinism wako katika hatari kubwa. Mratibu huyo amesema kwamba pamoja na
kupongeza juhudi za serikali katika kukabiliana na wimbi hilo la mauaji
hayo, Umoja wa Mataifa unataka Mamlaka husika kuhakikisha haki za raia
zinalindwa na utawala wa sheria unazingatiwa.
"
Tunataka mwaka 2015 kuwa mwaka ambapo haki za Watanzania wote
zitaheshimiwa wakiwemo albino" Taarifa imesisitiza. Mratibu huyo wa
umoja wa Mataifa amesema kwamba amezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Geita
Fatma Mwassa na chama cha Maalbino nchini TAS.
Amesema
Mkuu huyo wa mkoa alimhakikishia kwamba wanafanya kila linalowezekana
kukomesha madhila dhidi ya maalbino, huku TAS ikitaka kuhakikisha kwamba
huu ni mwaka wa kukomesha mauaji. Aidha Mratibu wa The Same Sun (UTSS)
nchini, Vicky Ntetema, amemweleza mratibu huyo wa Umoja wa Mataifa
mashaka yake wakati taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment