
Nchini
Syria zaidi ya Wakristo 80 wametekwa nyara kaskazini mashariki mwa nchi.
Inasadikiwa kuwa watu hao wametekwa nyara na wanamgambo wa makundi ya
kiislamu, baada ya kuvamia vijiji kadhaa katika mkoa wa Hassaké, mkoa
unaopiganiwa na wanajihadi, ambao uko mikononi mwa wapiganaji wa Kikurdi
kutoka Iraq.
Wengi mwa
wakazi wa vijiji hivyo wameyahama makazi yao, lakini makumi ya raia
hao, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, wanasadikiwa kutekwa nyara
na wanajihadi.
Kwa
mujibu wa shirika la haki za binadamu nchini Syria (OSDH) pamoja na
mashirika mengi ya Kikisto yanayoendesha harakazi zao Ulaya na Amerika
ya Kaskazini, wanamgambo wa kundi la wapiganaji wa Dola la kiislamu (IS)
wamevamia vijiji kadhaa vinavyopatikana kusini mwa mto Khabour, eneo
linalopatikana katika uwanja wa mapigano, ambalo linagawa wapiganaji wa
Kikurdi kutoka Syria na mahasimu wao wa IS.
Shambulio
hilo lilinaaminika kuwa limeendeshwa mapema Jumanne asubuhi wiki hii.
Familia kadhaa zilikimbia eneo hilo mapema, kwa kuhofia kuuawa na
wanamgambo hao. Hata hivyo wapiganaji wa IS wamewateka nyara watu walio
kati ya 90 na 200, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali.
Kwa mujibu wa shirika la misaada kwa raia wa Syria ADFA, wanaume wametenganishwa na wanawake pamoja na watoto.
Inaaminiwa
kuwa wapiganaji wa IS wameomba kubadilishana wafungwa na wapiganaji wa
Kikurdi wanaoshirikiana na wanamgambo wa Kikristo.
Kwa
mujibu wa taarifa ambayo tuliyonayo, mapigano makali yanaendelea katika
eneo hilo. Mapigano ambayo yalisababisha raia kuyahama makazi yao na
kukimbilia kaskazini na katika maeneo ya Wakurdi kutoka Syria, ambayo
yako mbali na wapiganaji wa Dola la Kislamu.CHANZO:I.R.F
No comments:
Post a Comment