Henry
Mdimu (katikati anayezungumza) akitoa ufafanuzi wa namna ya kutoa elimu
juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi 'Albino' huku kushoto akiwa
ni Mratibu wa Fedha na Udhamini wa Imetosha, Monica Joseph na Masoud
Kipanya ambaye naye ni mmoja wa wakilishi wa Imetosha.
Mwakilishi
wa Tanzania Bloggers Network, Joakhim Mushi (kushoto) akielezea namna
ya kuweza kusambaza taarifa ya kupinga ukatili dhidi ya mauaji ya Albino
kupitia vyombo vya habari.
Bango lenye ujumbe wa Imetosha.(P.T)
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini mkutano huo.
BALOZI wa
kujitolea wa harakati za imetosha, Henry Mdimu amezungumza na
wanahabari juu ya kukomesha mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi,
maarufu Albino unaoendelea hivi sasa .
Akizungumza
na wanahabari katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar, Mdimu alisema
kuwa dhumuni lake kuu ni kutaka kueleza ulimwengu kupitia vyombo
mbalimbali vya habari juu ya harakati ya ‘Imetosha’ambayo ameianzisha
yeye.
Alisema,
ameamua kuanzisha ishu hiyo baada ya kushuhudia ndugu zake wenye ulemavu
wa ngozi wakiteseka kwa muda mrefu huku akiongeza kuwa alishindwa
kuanzisha harakati hizo kwa kuviamini vyombo vinavyohusika na utetezi wa
watu wenye ulemavu wa ngozi.
Hata
hivyo, alisema ameamua kuweka jitihada zake binafsi ili kuisaidia
serikali kuondoa doa linaloichafua nchi hii yenye amani, hivyo amewaomba
Watanzania wote kushikamana kupinga ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu
wa ngozi.
Alitoa
ufafanuzi kwa kumnukuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete akisema kuwa kati ya mwaka 2006 hadi 2015,
watuhumiwa 139 wameshikiliwa ambapo kesi 35 zimeandikishwa huku
watuhumiwa 73 wakiachiwa huru na wengine 15 wamekamatwa na makosa hayo.
“Kutokana
na ushawishi nilionao kama mwandishi na mtangazji wa redio pia ni
Blogger, ninaamini nitaleta mabadiliko makubwa katika kuhakikisha haki
ya kuishi kwa ndugu zangu inaheshimiwa na kubaki kama walivyo watu
wengine.
“Nina
mpango wa kwenda Kanda ya Ziwa kuhangaika na hili mpaka nione mwisho
wake kwani tatizo ni rahisi kulimaliza kabla halijaenea nchi nzima maana
walemavu wapo nchi nzima lakini kabla ya hapo Machi 21, mwaka huu
kutakuwa na matembezi ya hisani ya kilomita tano hapa jijini Dar ya
kupinga ukatili huo ambayo yataanzia katika viwanja vya Leaders kupitia
Kinondoni Manyanya na kurudi viwanjani hapo .
“Mimi
pamoja na wanaharakati wenzangu tutaondoka kuelekea Mwanza kwa ajili ya
kutoa elimu kwa njia ya sanaa tukiwa na washauri nasaha pamoja na
wasanii wa muziki wanaoandaa nyimbo mabalimbali zenye ujumbe wa
kutokomeza ukatili huu,” alisema Mdimu.
No comments:
Post a Comment