Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Jimbo la
Kongwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mkoka,wilaya ya Kongwa
mkoani Dodoma ikiwa sehemu ya muendelezo wa ziara zake za kukagua
utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2010.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mkoka
wilayani Kongwa na kuwaambia moja ya sifa muhimu na ya kipekee kwa
kiongozi anayefaa kuongoza wananchi ni Uadilifu.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wananchi
waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikuwa mgeni wa Heshima, Kimbisa
aliwaambia wana CCM kuwa Dodoma itakuwa mfano katika kutenda haki.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mkoka wilaya
ya Kongwa mkoani Dodoma ambapo aliwaambia wananchi hao CCM ni Chama
pekee chenye kujali Watanzania kinachosimamia na kuitunza amani
iliyokuwepo
Mpwapwa.Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana amesema kitu kitakachokiokoa chama hicho ni wanachama
kutowafumbia macho wezi na mafisadi akisisitiza kuwa kulindana na upole
kutakiangamiza chama hicho kikongwe.
Kinana amesema hayo wakati CCM ikizidi kuchafuliwa
na kashfa za ufisadi ambazo zimekuwa zikiwakabili makada wake ambao
mara kadhaa wamelazimika kuachia ngazi baada ya Bunge kukomaa kutaka
hatua zichukuliwe.
Tayari makada wa CCM wameshalazimika kuwajibika
katika kashfa za uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow ambako
zaidi ya Sh306 bilioni zilichotwa, kashfa ya Akaunti ya Malipo ya Madeni
ya Nje (EPA), kashfa iliyoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG), kashfa ya rada na nyingine kwenye sekta ya utalii.
Tayari makada wa CCM wameshalazimika kuwajibika
katika kashfa za uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow ambako
zaidi ya Sh306 bilioni zilichotwa, kashfa ya Akaunti ya Malipo ya Madeni
ya Nje (EPA), kashfa iliyoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG), kashfa ya rada na nyingine kwenye sekta ya utalii.
Kinana, ambaye amekuwa akishambulia viongozi wa
Serikali kwenye ziara zake, alitoa agizo hilo juzi wakati alipokuwa
akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Kibakwe wilayani
Mpwapwa ambako alisema kufanya hivyo ndiyo salama ya CCM.
“Tatizo lenu (wanachama wa CCM) mnakuwa wapole na
mnajenga tabia ya kulindana. Kwa njia hiyo hamtaweza kukisaidia chama
chenu. Mtu akikosea hakuna bahati mbaya, ondoa huyo na apelekwe jela
mara moja ili kazi nyingine zisonge,” alisema Kinana ambaye hata hivyo
hujiepusha kuzungumzia kashfa hizo kubwa kwenye mikutano yake.
Kwa upande mwingine alisema kuwa ndani ya CCM kuna
baadhi ya wanachama wezi ambao alidai hawajai kiganja kati ya wanaCCM 7
milioni, lakini wamesababisha wanaCCM kudharauliwa na kuwakosesha raha
maskini wengi walioko vijijini ambao alisema wanaendelea kutukanwa kuwa
ni mafisadi jambo ambalo siyo kweli.
Huku akishangiliwa na umati mkubwa uliohudhuria
mkutano huo, alisema dhambi mbaya kwa sasa ni ile ya kufanya kazi kwa
mazoea na kulindana kwa kisingizio cha utawala bora wakati wezi wanaiba
bila ya kuangalia masuala ya utawala bora.
Kauli ya Kinana huenda ikawapa nguvu baadhi ya
wabunge ambao wamekuwa wakisimama kidete kwa ajili ya kupinga ufisadi,
lakini mara kadhaa wakiwa bungeni hushindwa katika mapambano yao
kutokana na misimamo ya chama.
Kinana alisema suala la wanachama wa CCM kuimba
“iyena iyena” huku wakiwa wapole huu siyo wakati wake badala yake
wabadilike na kukemea maovu na mambo yanayokwenda kinyume na chama chao.
“Nasema kwa wanachama wa CCM nchi nzima, mpango
wa kuhamisha mtu kutoka eneo moja na kupelekwa sehemu nyingine huo
usiwepo, mtu akituhumiwa lazima aachie ngazi akisubiri uchunguzi,”
alisema na kuongeza.
“Wakati wa kuiba wezi hawafuati utawala bora,
lakini wanapotakiwa kuondoka ndipo masuala ya utawala bora yanapoanza
kusimama, naona suala la utawala bora litazamwe upya maana wengine
hawafanyi kama tulivyowatuma.”
No comments:
Post a Comment