Mwanamke
wa Tunisia akibeba bango lililoandikwa kwa herufi za ishara ya damu
mjini Tunis: " hapana kwa ugaidi" , Machi 19 mwaka 2015.
Na RFI
Maandamano
mapya yanayojumuisha mamia ya watu yanatazamiwa kufanyika Ijumaa wiki
hii katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, mbele ya makavazi ya Bardo jijini
Tunis, ambapo shambulio la kigaidi liligharimu maisha ya watu 21.
Raia wa
kigeni 20 pamoja na raia mmoja wa Tunisia ni miongoni mwa waliouawa.
Watu zadi ya arobaini walijeruhiwa katika shambulio hilo.
Awali
maandamano kama hayo yaliandaliwa na asasi thelathini pamoja na chama
kikuu cha wafanyakazi nchini Tunisia (UGTT), huku kauli mbio ikiwa "
Umoja wa kitaifa"dhidi ya ugaidi.
Rais wa
Tunisia Beji Caïd Essebsi, kwa upande wake ametangaza kwamba wauaji
walioendesha shambulio hilo katika makavazi ya Bardo walikua walivalia "
vilipuzi" na vikosi vya usalama viliwahi kuzima shambulio hilo kwa "
kuepuka janga kubwa" ambalo lingeweza kutokea kutokana na vilipuzi
hivyo.
Baadhi ya waandamanaji waliweka shada za maua na mishumaa kwenye eneo la tukio kwa kutoa rambirambi zao kwa wahanga.
Mokthar
Trifi, kiondozi wa zamani wa shirika la haki za binadamu nchini Tunisia,
ambaye alikua alishiriki maandamano hayo alisema raia wote wa Tunisia
wameungana na kusema " hapana" kwa ugaidi.
Kundi la
wapiganaji wa Dola la Kiislamu limekiri kutekeleza shambulio hilo dhidi
ya makavazi ya Bardo mjini Tunis, lililogharimu maisha ya watu 21, wengi
wao wakiwa watalii.
Washukiwa
tisa walikamatwa Alhamisi wiki hii, kwa mujibu wa Ikulu ya Tunis. Watu
hao wanasadikiwa kuwa walikua wakiwasiliana na wauaji hao walioendesha
shambulio katika makavazi ya Bardo.
No comments:
Post a Comment