Picha inaonyesha helikopta ya mashambulizi ya MONUSCO, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo.
Na RFI
Mvutano
baina ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC) umechukuwa sura nyingine hapo jana katika Baraza la Usalama
la umoja huo kuhusu kuondoka au la kwa vikosi vya kulinda amani nchini
humo MONUSCO.
Waziri wa
Mambo ya Nje wa Congo Raymond Tshibanda amesema kuwa wakati umefika kwa
nchi yake kuwajibika kikamilifu kwa ajili ya usalama wa nchi yake
akiliomba baraza hilo kuheshimu dhamira ya serikali ya Kinshasa kwa
kuamuru MONUSCO waanze kuondoka kwa awamu.
Aidha,
waziri huyo amesema kuwa maendeleo ya kisiasa na kiuchumi yaliyoletwa na
serikali yake ni mafanikio makubwa, huku akidai kuwa makabiliano ya
vikosi vya serikali dhidi ya waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR mashariki
mwa DRC yanaendelea kushika kasi.(P.T)
Akizungumza
kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa
Umoja wa mataifa na mkuu wa vikosi hivyo vya MONUSCO, Martin Kobler,
amesisitiza kwamba kwa ujumla hali ya usalama imeimarika na kwamba bado
yako maeneo mengi ya kufanyia kazi mashariki mwa nchi hiyo ambako raia
wanaishi katika hofu.
Kulingana
na vyanzo vya kidiplomasia, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lina
mpango wa kupunguza vikosi hivyo kwa kiwango cha askari elfu mbili kati
ya elfu ishirini walioko Congo wakati serikali ya Kinshasa ikisema
kiwango cha kwanza cha wataokaoondoka kitakua cha askari elfu sita.
No comments:
Post a Comment