ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label FREEMAN MBOWE. Show all posts
Showing posts with label FREEMAN MBOWE. Show all posts

Sunday, May 11, 2014

UKAWA WAPIGWA MARUFUKU BUNGE LA BAJETI


Friday, November 29, 2013

Baregu aitahadharisha Chadema kuhusu Zitto

“Tuhuma zinazotolewa dhidi ya Zitto na wenzake kwamba wamenunuliwa na chama fulani cha siasa zinahitaji maelezo na vielelezo vya kina ili kuwaaminisha wengi. Nasema hivi kwa sababu historia yao inadhihirisha kuwa wana uchungu na chama chao. Chama kinachoongozwa kwa demokrasia na kinachotarajiwa kushika madaraka ya kuongoza nchi, lazima kionyeshe uwezo mkubwa wa kuvumiliana, kutafakari, kusamehe, kuaminiana na kujenga umoja wenye lengo la kuelekea kusudio lake.” Baregu  
Dar es Salaam. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amewataka viongozi wa chama hicho kutafakari na kudhibiti madhara yanayoweza kukikumba hasa baada ya hatua yake ya hivi karibuni ya kumvua nyadhifa zote, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili.
“Bahati nzuri wamevuliwa uongozi siyo uanachama, binafsi nadhani  viongozi wanatakiwa kutafakari na kudhibiti madhara zaidi kwa chama, wakishupaza shingo, lolote litakalotokea watakuwa ni sehemu ya lawama,” Profesa Baregu alisema Dar es Salaam jana.
Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walivuliwa uongozi Novemba 22 mwaka huu, kwa tuhuma za kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho kinyume na katiba, sheria na itifaki za chama.
Profesa Baregu alisema pamoja na viongozi hao kuvuliwa madaraka, mema waliyokifanyia chama hicho hayawezi kuyeyuka na kwamba makosa yao yasikuzwe kiasi cha kufuta mazuri yao katika kujenga chama hicho.
“Ni vigumu kuamini kwamba makosa ya Zitto, Dk Kitila na Samson Mwigamba yanaweza kuyeyusha mema waliyokifanyia chama kama barafu inavyoyeyuka juani.”
Profesa Baregu ambaye alikuwapo katika kikao kilichowavua uongozi Zitto na wenzake alisema kinachotakiwa kufanyika sasa ni kujenga uhusiano ndani ya chama na hasa kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ambao umeanza Novemba 22 na unatarajiwa kumalizika Juni mwakani.
Alitaka hatua dhidi yao zizingatie Katiba ya chama hicho ili kuhakikisha kuwa hazivurugwi na mamlaka nyingine zilizopo ndani ya Chadema akisema mkutano wa Baraza Kuu unaweza kubadili uamuzi wa Kamati Kuu.
“Kinachotakiwa kufanywa ni kuwatangazia wanachama misingi, taratibu na kanuni za kuzingatia katika harakati zao  ili kuondoa hali ya watu kufanya mambo kwa kificho,” alisema na kuongeza:
“Ni wazi wengi wapo katika kampeni, ichukuliwe kuwa walioshughulikiwa wamebambwa na iwe njia ya kuonyesha ukomavu katika kustahamiliana.”
Alisema asingependa kuona siasa za kulipizana visasi na kusisitiza kwamba hata kama mwanachama ana chuki binafsi na mwenzake, hatakiwi kutumia chuki hiyo kumhukumu.
“Tuhuma zinazotolewa dhidi ya Zitto na wenzake kwamba wamenunuliwa na chama fulani cha siasa zinahitaji maelezo na vielelezo vya kina ili kuwaaminisha wengi. Nasema hivi kwa sababu historia yao inadhihirisha kuwa wana uchungu na chama chao. Chama kinachoongozwa kwa demokrasia na kinachotarajiwa kushika madaraka ya kuongoza nchi, lazima kionyeshe uwezo mkubwa wa kuvumiliana, kutafakari, kusamehe, kuaminiana na kujenga umoja wenye lengo la kuelekea kusudio lake.”CHANZO MWANAINCHI

Tuesday, November 12, 2013

SALAMU ZA RAMBIRAMBI TOKA CHADEMA KWA KIFO CHA DK MVUNGI

 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ametuma salaam za rambirambi ya kifo cha Dkt. Edmund Sengondo Mvungi, akitoa pole kwa familia, uongozi na wanachama wa NCCR-Mageuzi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Akitoa kauli hiyo kwa niaba ya CHADEMA na wanachama wa chama hicho, Mwenyekiti Mbowe amesema kuwa amepokea kwa masikitiko na mshituko mkubwa taarifa za kifo cha Dkt. Mvungi, akimwelezea kuwa alikuwa mwanasiasa mwenye msimamo ambaye hakuwahi kutetereka kusimama na chama chake tangu alipojiunga nacho na kuanza kushiriki siasa za mageuzi nchini. “Kwa niaba ya CHADEMA na wanachama wetu nchi nzima, napenda kutoa salaam za pole sana kwa familia ya marehemu, mjane na watoto. Natoa pole kwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na wanachama wa chama hicho, pia tunatoa pole kwa Jaji Mstaafu Joseph Warioba na makamishna wote wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwakifo cha Dkt. Mvungi. Tunaomba Mwenyezi Mungu awatie nguvu sana wakati huu wa majaribu na majonzi makubwa. “Dkt. Mvungi alikuwa mwanasiasa mwenye misimamo ambaye hakuwahi kukihama chama chake tangu alipoanza siasa za mageuzi nchini. Ni kati ya wasomi wachache waliokuwa na ujasiri na kuthubutu kujiunga na vyama vya upinzani tangu mapema. "Mvungi pia alikuwa mmoja wa wanasiasa wa mwanzo kabisa kupigania nchi yetu iwe na Katiba Mpya, ili hatimaye siasa zetu, hususan demokrasia ya vyama vingi nchini iendeshwe kwa misingi iliyo imara,” amesema Mwenyekiti Mbowe na kuongeza; “Mwenyezi Mungu alimjalia marehemu akaweza kushiriki kutimiza ndoto hiyo baada ya kuteuliwa kuwa mmoja wa makamishna wa Tume ya Mpya, kazi ambayo ameifanya hadi siku alipokutwa na tukio lililosababisha mauti yake.” Mwenyekiti Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, amesisitiza kuwa kwa namna ambavyo Dkt. Mvungi alikuwa mstari wa mbele katika suala hilo, Tume ya Katiba Mpya inao wajibu wa kuthamini mchango wake katika hatua iliyofikia sasa ya mchakato huo nyeti hadi utakapofika mwisho. “Wakati tukimwombea marehemu kwa Mungu, alazwe mahali pema peponi, ni matumaini yetu kuwa serikali kupitia vyombo vyake itahakikisha kuwa wale wote waliohusika katika tukio la lililosababisha kukatisha uhai wa Dkt. Mvungi wanapatikana na kuchukuliwa hatua zote zinazostahili kisheria,” amesema Mwenyekiti Mbowe.

Thursday, September 26, 2013

VYAMA VYA UPINZANI VYAENDELEA NA MKUTANO WA KATIBA MPYA ZANZIBAR HAPO JANA


Mshikamano: Wenyeviti wa vyamba vya upinzani nchini wakishikana mikono kuonyesha mshikamano kabla ya kuanza mkutano kwenye Uwanja vya Kibandamaiti, Zanzibar jana.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto) akiteta jambo la Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Joseph Mbatia wakati wa mkutano wa kuungwa mkono na wananchi katika upatikanji wa katiba mpya.
Umati: Wananchi waliohudhuria mkutano huo wa kutafuta katiba mpya.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akihutubia wananchi wakati wa mkutano wa kuungwa mkono na wananchi katika upatikanaji wa katiba mpya.
Lipumba akisalimiana na Mbowe.Kwa hisani ya Global Publishers Blog

Monday, September 16, 2013

Wenyeviti wa vyama vya upinzani wakiwa pamoja, na kwa sauti moja.

 

Wenyeviti wa vyama vya upinzani wamekaa pamoja wakipinga muswada wa katiba usipitishwe. Wakuu hao wa vyama mbalimbali vya siasa na wenye ushawishi mkubwa kwa wamanchi wanakutana pamoja kwa jambo moja tu huku kila mmoja akiwa na tofauti na mwenzake. Watasimama pamoja katika hili la katiba lakini wametofautiana kwa mengi na kila mmoja wao ana nia ya kushika hatamu za uongozi wa nchi hii ya Tanzania. Kama wanavyoungana kwa ajili ya kuupinga mswada wa katiba basi wangewekeza kwenye kuondoa tofauti zao ili waungane kwenye uchaguzi. Wote wasarende uongozi wao na katiba zao wachague uongozi mpya wa muungano waweke mgombea mmoja wa urais. Wakifanya hivi naamini watakuwa wanawatendea haki Watanzania na wapiga kura watakuwa na wakati mzuri wa kuchagua viongozi bora na Wananchi wengi watajitokeza kupiga kura kwa kuwa kutakuwa na ushindani wa ukweli. Tutaingia kwenye kupiga kura bila kuwa na uhakika ni nani ataibuka mshindi, na atakayechaguliwa atakuwa anawakilisha wananchi wote.  Utengano wa wanasiasa ndio unaofanya wapiga kuwa wawe wachache. Pengine kupiga kura inakuwa kama si jambo la kishindani, unajua atakayeshinda anatoka chama fulani, so uchaguzi unakuwa kama ushahidi tu. Hii inasababishwa na ubinafsi wa vyama vya upinzania. Tupeni haki ya Demokrasia na sio kututengatenga kadiri mnavyotaka.

Friday, September 6, 2013

VURUGU ILIYOTOKEA BUNGENI SEPTEMBA 5/2013 WAKATI WA MATUKIO YA VURUGU KATI YA ASKARI WA BUNGE NA WABUNGE WA CHADEMA MJINI DODOMA.




vurugusugu_dd67c.jpg
Hapa askari wa bunge wakipambana na mhe Joseph Mbilinyi huko mhe akiwa ameshika mkono wa kipaza sauti kufuatia kutoelewana ndani ya ukumbi wa bunge jana.
SUGU AKIDHIBITIWA NA ASKARI WA BUNGE NDANI YA UKUMBI WA BUNGE HUKU AKIWA AMENG'ANG'ANIA KIPAZA SAUTI.
MHE SUGU WAKIMZUIA.
MHE JAMES MBATIA AKIWA NA MSHANGAO.
HAPA MHE MBOWE WAKIJADILI JAMBO.CHANZO YA YOTE KIINI KIMEANZIA HAPA.
MSHANGAO


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...