ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label Zitto Kabwe. Show all posts
Showing posts with label Zitto Kabwe. Show all posts

Thursday, March 12, 2015

Zitto Kabwe Asisitiza Kuwa Yeye ni Mbunge Halali wa Kigoma Kaskazini.....Asema Hana Taarifa ya Kuvuliwa Uanachama CHADEMA.


Siku moja baada ya mahakama kuu kutupilia mbali ombi la mbunge wa Kigoma kaskazini Mh Zitto Kabwe kujadiliwa na vikao vya Chadema kuhusu hatma ya uanachama wake na kutakiwa kulipagharama za kesi hiyo mbunge huyo amedai kuzisikia taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari lakini hana taarifa rasmi.
Hayo ndio yalikuwa majibu ya awali ya mbunge huyo wa Kigoma kaskazini alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya mahakama kutoa uamuzi wake haraka mwanasheria mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Mh Tundu Lisu akazungumza na vyombo vya habari kuhusu Chadema kutomtambua Mh Zitto kama mwanachama wa chama hicho ambapo ili kusikia kauli ya Mh Zitto kuhusu suala hilo ITV ikafika katika ofisi ndogo za bunge zilizoko jijini Dar es Salaam na kumshuhudia Mh Zitto akiongoza vikao vya kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu ya mashirika ya uma PAC ambapo baada ya kumalizika kwa kikao hicho akazungumzia maamuzi hayo ya mahakama na Chadema baada ya kuhojiwa na waandishi wa habari.
Aidha kutokana na madai hayo Mh Zitto amesema kwa kuwa hana taarifa rasmi ijumaa ya wiki hii atakwenda jimboni kwake kuzungumza na wananchi wa jimbo lake kama mbunge na kisha jumanne ya wiki ijayo atahudhuria vikao vya bunge kama kawaida na kuongeza kuwa tukio hilo linamkomaza kisiasa na kwamba siasa zake ni zakujadili masuala na si watu kama walivyo baadhi ya wanasiasa wenzake.
Pia amezungumzia hatma ya mustakabali wake kisiasa na kuelezea mahusiano yake na chama cha demokrasia namaendeleo Chadema kwa sasa.
Source: ITV

Friday, November 29, 2013

Baregu aitahadharisha Chadema kuhusu Zitto

“Tuhuma zinazotolewa dhidi ya Zitto na wenzake kwamba wamenunuliwa na chama fulani cha siasa zinahitaji maelezo na vielelezo vya kina ili kuwaaminisha wengi. Nasema hivi kwa sababu historia yao inadhihirisha kuwa wana uchungu na chama chao. Chama kinachoongozwa kwa demokrasia na kinachotarajiwa kushika madaraka ya kuongoza nchi, lazima kionyeshe uwezo mkubwa wa kuvumiliana, kutafakari, kusamehe, kuaminiana na kujenga umoja wenye lengo la kuelekea kusudio lake.” Baregu  
Dar es Salaam. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amewataka viongozi wa chama hicho kutafakari na kudhibiti madhara yanayoweza kukikumba hasa baada ya hatua yake ya hivi karibuni ya kumvua nyadhifa zote, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili.
“Bahati nzuri wamevuliwa uongozi siyo uanachama, binafsi nadhani  viongozi wanatakiwa kutafakari na kudhibiti madhara zaidi kwa chama, wakishupaza shingo, lolote litakalotokea watakuwa ni sehemu ya lawama,” Profesa Baregu alisema Dar es Salaam jana.
Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walivuliwa uongozi Novemba 22 mwaka huu, kwa tuhuma za kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho kinyume na katiba, sheria na itifaki za chama.
Profesa Baregu alisema pamoja na viongozi hao kuvuliwa madaraka, mema waliyokifanyia chama hicho hayawezi kuyeyuka na kwamba makosa yao yasikuzwe kiasi cha kufuta mazuri yao katika kujenga chama hicho.
“Ni vigumu kuamini kwamba makosa ya Zitto, Dk Kitila na Samson Mwigamba yanaweza kuyeyusha mema waliyokifanyia chama kama barafu inavyoyeyuka juani.”
Profesa Baregu ambaye alikuwapo katika kikao kilichowavua uongozi Zitto na wenzake alisema kinachotakiwa kufanyika sasa ni kujenga uhusiano ndani ya chama na hasa kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ambao umeanza Novemba 22 na unatarajiwa kumalizika Juni mwakani.
Alitaka hatua dhidi yao zizingatie Katiba ya chama hicho ili kuhakikisha kuwa hazivurugwi na mamlaka nyingine zilizopo ndani ya Chadema akisema mkutano wa Baraza Kuu unaweza kubadili uamuzi wa Kamati Kuu.
“Kinachotakiwa kufanywa ni kuwatangazia wanachama misingi, taratibu na kanuni za kuzingatia katika harakati zao  ili kuondoa hali ya watu kufanya mambo kwa kificho,” alisema na kuongeza:
“Ni wazi wengi wapo katika kampeni, ichukuliwe kuwa walioshughulikiwa wamebambwa na iwe njia ya kuonyesha ukomavu katika kustahamiliana.”
Alisema asingependa kuona siasa za kulipizana visasi na kusisitiza kwamba hata kama mwanachama ana chuki binafsi na mwenzake, hatakiwi kutumia chuki hiyo kumhukumu.
“Tuhuma zinazotolewa dhidi ya Zitto na wenzake kwamba wamenunuliwa na chama fulani cha siasa zinahitaji maelezo na vielelezo vya kina ili kuwaaminisha wengi. Nasema hivi kwa sababu historia yao inadhihirisha kuwa wana uchungu na chama chao. Chama kinachoongozwa kwa demokrasia na kinachotarajiwa kushika madaraka ya kuongoza nchi, lazima kionyeshe uwezo mkubwa wa kuvumiliana, kutafakari, kusamehe, kuaminiana na kujenga umoja wenye lengo la kuelekea kusudio lake.”CHANZO MWANAINCHI

Wednesday, November 27, 2013

MTEI ASEMA "WASALITI WOTE TUTAWAFUKUZA CHADEMA".

Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei amesema kuwa chama hicho kitaendelea kuwafukuza wote wanaokihujumu huku akieleza kwamba, anaunga mkono kuvuliwa uongozi kwa Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu , nyumbani kwake jana, Mtei aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu (BOT) na Waziri wa Fedha katika utawala wa awamu ya kwanza wa Mwalimu Julius Nyerere, aliweka wazi kuwa daima ataunga mkono dhamira ya kukisimamia chama hicho aliyoitaja kuwa ni safi.

 “Naunga mkono uamuzi wote wa Kamati Kuu, kuwasimamisha na kuwavua uongozi Naibu Katibu Mkuu wetu Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo. Na kwa sababu Chadema inataka kusonga mbele, lazima iwafukuze mafisadi na wezi wanaoshirikiana kukihujumu chama,” alisema Mtei.

Bila kufafanua zaidi au kutaja majina, mwenyekiti huyo wa kwanza wa Chadema alisema: “Hatuwezi kuendesha chama wakati viongozi wengine wanapokea pesa na kuzihifadhi kwenye akaunti za siri.” Alisisitiza kwamba kwa nafasi yake akiwa mwasisi wa Chadema ni lazima ahakikishe anaunga mkono dhamira safi ya kukisimamia chama.

Kuhusu Arfi kujiuzulu

Akizungumzia hatua ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Saidi Arfi kujiuzulu, Mtei alisema kuwa inafaa kiongozi huyo ajitazame upya na kujisahihisha badala ya kuwa mlalamikaji kila siku.

“Aache kulalamika kwa sababu, wakati alipochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti mimi nilisimamia uchaguzi. Kama alikuwa na ndoto kwamba siku moja atakuwa mwenyekiti wa Chadema taifa alipaswa kujichunguza kwanza,” alisema.

Mtei aliongeza kuwa iwapo kuna watu wanadhani Chadema itakufa hiyo ni dhana potovu, lakini kwa sasa chama hicho kimejipanga kuchukua dola na tayari wamejiimarisha kimkakati.

“Katika suala la kushughulikia watu wanaokihujumu chama  hakuna ‘compromise’ (mjadala),” alihitimisha Mtei.   Juzi Chadema ilitangza uamuzi wa Kamati Kuu yake kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dk Kitila, huku Arfi akitangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara.

Mtei amewahi kumkemea na kumwonya Zitto katika mambo mbalimbali aliyofanya ndani ya Chadema, moja ikiwa Oktoba mwaka jana ambapo mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, alipotangaza kuwania urais mwaka 2015.

Alisema kuwa hatua hiyo itasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama,  huku akiongeza kwamba amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana-Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.

“Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga,” alisema Mtei.

Mtei alisema hatua ya mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015, imekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema, akiweka wazi kuwa wakati ukifika chama hicho kitafanya uchaguzi sahihi.

“Siyo vibaya kwa Zitto kuonyesha hisia zake, lakini ndani ya Chadema kwa sasa, kuna watu mbalimbali wanaopenda kuwania urais, lakini hawajatangaza. Dk Slaa (Willbrod) anataka, Freeman (Mbowe) anataka, Zitto anataka, hata mimi huenda nikataka kugombea. Hapa hakuna upendeleo, sifa ndizo zitakazoamua,” alisema.

Hata hivyo, Zitto alipinga kauli hiyo akisema: “Demokrasia haileti mizozo kwenye vyama vya siasa hata siku moja,  bali humaliza mizozo. Udikteta, kuminya fikra huru na mawazo huru, ndivyo huleta mizozo kwenye vyama vya siasa.”

Alisema ni muhimu wazee wakawaacha vijana wawe huru kusema wanachofikiri, kwa kuwa uhuru wa fikra na mawazo ni moja ya haki za msingi na moja ya nguzo za demokrasia.

“Ninarudia, nitaomba kupeperusha bendera ya chama changu kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2015.  Naamini kwamba ninaweza kuwezesha chama chetu kushinda na kuongoza dola na Chadema kutoa rais wakati baadhi ya waasisi wetu wakiwa hai na kuona vijana wao tunavyobadili maisha ya Watanzania na kutimiza ndoto zao,” alisema Zitto.

Alisema ana uwezo, uadilifu na uzalendo wa kutosha kuwa Amiri Jeshi Mkuu na kuunganisha Watanzania kuwa wamoja bila kujali rika, dini wala makabila yao... “Nimejiandaa kisaikolojia kukabili changamoto za ufukara wa nchi yetu.”

Thursday, November 21, 2013

ZITTO NA KITILA wadaiwa KUVULIWA VYEO VYOTE NDANI YA CHAMA !

Kikao cha Kamati Kuu ndiyo kimeisha muda huu, na taarifa zilizopo ni kwamba kambi ya PM7 imevunjwa rasmi baada ya viongozi wake kuvuliwa vyeo vyote walivyo navyo ndani ya chama.
Waliovuliwa vyeo ni Zitto Kabwe, ambaye amevuliwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa chama pamoja na nafasi ya Naibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Dr. Kitila Mkumbo yeye amevuliwa nafasi ya mjumbe wa kamati kuu.

  Kamati Kuu imewaandikia barua Zitto na Kitila, wajieleze ndani ya siku 14 kwanini wasifukuzwe uanachama.

Tunawapongeza kamati kuu kwa hatua hii muhimu kwa mustakbali wa chama na taifa. 

CHANZO: JAMII FORUM 

Tuesday, August 27, 2013

Zitto: Sitogombea Urais wala Ubunge 2015



MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili.
Bw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015. 
Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi ya pili katika mchujo huo ambapo Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba, alishika nafasi ya kwanza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwanasiasa aliyeshika nafasi ya tatu katika mchujo huo alikuwa Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam, Bw. John Mnyika (CHADEMA).
"Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na siasa kwani nimechoka nazo, nitatafuta chuo nikafundishe na kama nitakosa ni bora nikalime michikichi... sihitaji urais," alisema. 
Katika mkutano wa wanafunzi hao, walisema Bw. Makamba ana sifa zote za kuwa rais wa nchi kamaatagombea nafasi hiyo mwaka 2015 ili aweze kulikomboa Taifa ambalo hivi sasa linakabiliwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani. 
Wanafunzi hao walikwenda mbali zaidi na kuyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni pamoja na vurugu, kutekwa kwa watu wasio na hatia, kufanyiwa vitendo vya ukatili, kumwagiwa tindikali na kupungua kwa mtangamano wa kijamii. 
Mwenyekiti wa mkutano huo ambao ulifanyika mkoani Morogoro ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Mbeya, Bw. Theonest Theophil, alisema Bw. Makamba alipata kura 72 ambapo Bw. Kabwe alipata kura 20.
Bw. Theophil alisema sifa za kiongozi wanayemtaka kwanza awe kijana mwenye fikra mpya, atakayeleta matumaini mapya, kuwaunganisha Watanzania, asiyeendekeza siasa za kikanda, mdini na mkabila. 
Sifa nyingine ni kiongozi mwadilifu asiye na rekodi ya kutuhumiwa mahali popote kwa vitendo viovu, mtulivu, mwenye busara na anayepima kauli zake.

Source: Majira

Friday, April 26, 2013

ZItto Kabwe na na Joshua Nassari watoa masikitiko yao kuhusu kukamatwa kwa Mbunge wa Arusha Godbless Lema


 
Nimepata kwa mshtuko na nikakataa kuamini kama ni kweli kuwa polisi wa Arusha wamevamia na kuizingira nyumba ya mbunge mwenzangu wa Arusha, Lema.

Nimelazimika kumpigia simu RPC kuthibitisha na cha ajabu akaniambia ni kweli.

Nimemshauri kama kiongozi mwenzake mwenye dhamana ya kusaidia kuilinda
kweli na haki ili kuleta Amani ya kweli kwenye mkoa wangu wa Arusha. Sidhani kama ni busara kutaka kuvamia nyumbani kwa Raia mwema achilia mbali Kiongozi mkubwa kama mbunge. "Kama watawala wanafanya hivi kwa mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu" itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida anayeishi usa river au unga ltd? Ukifuatilia na kuangalia video ya tukio la uhasibu chuoni arusha, utagundua makosa ya mtawala mkuu wa mkoa, ambaye kimsingi ni mkiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuwa sehemu ya sababu ya uvunjifu wa amani, kutokujua hata kusoma saikolojia ya watu.

Nyumbani kwa mbunge hakai mbunge mwenyewe. Kuna watoto akiwemo mwenye umri wa miezi mitano, mke, ndugu etc. Utapigaje mabomu kwenye nyumba hii, bila shaka yatakuwa mauaji. Lema si jambazi, ni kiongozi, ni role model, ni raia mwema sana na mzalendo kwa taifa lake.

Hii wapi sababu ya kuvamia kwake usiku na kuwapa wanafamilia pychological tortue.

Kama amenielewa atasikia, otherwise "truth will always stand" . Tuko tayari na tulishakuwa tayari, hatujashtukizwa. Tunaendelea kuongezewa kura za madiwani arusha juni 16, 2013. Ni vyema watawala wakakumbuka habari ya Farao na Mungu juu ya mateso ya wana wa Israel utumwani. "Mungu akaufanya moyo wa farao kuwa mgumu, ili azidi kujidhihirisha kwa wana wa Israel"
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...