ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label HESLB. Show all posts
Showing posts with label HESLB. Show all posts

Thursday, October 10, 2013

MULUGO ATAKA WALIOKOSA MIKOPO KUJISOMESHA

148 Philipo-Mulugo1 57d1b
Na Gladness Theonest
Serikali imewataka wanafunzi waliokosa mikopo kwa ajili ya masomo vyuo vikuu kurudi nyumbani na ikiwezekana wakauze viwanja au ng'ombe ili waweze kujisomesha kwani bajeti iliyopo haitoshi.Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo,wakati akizungumza na wanafunzi waliokosa mikopo ambapo kwa takriban wiki nzima wamepiga kambi wizarani hapo.(hd)
"Kasungura kadogo na mkumbuke kuwa mkopo ni kuomba kuna kupata na kukosa...hivyo wale waliokosa na walikuwa na vigezo watafute watu wengine wenye uwezo wawasomeshe kwa mwaka mmoja na unaofuata watume tena maombi," alisema.
Alisema kilio chao amekisikia na leo atazungumza na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusiana na malalamiko yao ambapo suala hilo litapelekwa Bungeni ili kujadiliwa.
"Kama Bunge litaamua kupunguza fedha kutoka kwenye bajeti zingine ili kusomesha wanafunzi hao. Bunge litaamua kwani Serikali ina nia nzuri sana kwani hadi sasa imetoa trilioni 1.5, lakini ndugu zenu hawarudishi," alisema.
Alitaja sababu nyingine ya wanafunzi kukosa mikopo ni Serikali kuangalia uhitaji, kwani kuna masomo maalumu walilenga hasa fani zenye upungufu wa wataalamu.
Alitaja fani hizo kuwa ni ualimu, udaktari na wahandisi. Alitaja sababu nyingine za wanafunzi kukosa mikopo hiyo ni waombaji kukosea majina na vitu vingine vidogo vidogo na walipotangaziwa kwenye vyombo vya habari warudi kurekebisha fomu zao hawakufanya hivyo.
Alisema waliokosea kujaza fomu hizo walikuwa 6,000 lakini waliorudi kufanya marekebisho walikuwa ni 3,000 na wengine 2,000 walikuwa na vigezo lakini wamekosa kutokana na sungura kuwa mdogo (bajeti).
Wanafunzi waliokosa mikopo walisema kama wenzao wameweza kupata mikopo kwa asilimia 100 basi waangalie namna ya kugawana ili wote waweze kupata
CHANZO MAJIRA

Wednesday, September 25, 2013

ZAIDI YA WANAFUNZI 300 WA VYUO VIKUU WATAKOSA MIKOPO



zzzzkawambwa_17ff6.jpg
Zaidi ya wanafunzi 300 wa elimu ya juu wa vyuo mbalimbali watakosa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kutokana na kushindwa kujaza fomu za kuomba mikopo katika kipindi kilichowekwa.Watakaokosa mikopo hiyo kwa mwaka wa masomo wa 2013/2014 ni kuanzia mwaka wa pili na kuendelea, ambao hawakujaza fomu za kuonyesha taarifa zao mpya kwa bodi.
Wanafunzi hao walitakiwa kuwasilisha maombi ya kupewa mikopo kati ya Mei hadi Julai 30, mwaka huu.
Mkugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HELSB, Cosmas Mwaisobwa, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi kuhusu utendaji wa kazi wa bodi hiyo.(P.T)
Mwaisobwa alisema kwa kuwa wanafunzi hao hawakujaza fomu za kuomba mikopo, mwaka huu hawatapata fursa hiyo na kwamba kwa mujibu wa utaratibu wao, kila mwaka lazima mwanafunzi aombe.
Alisema wanafunzi watakaokosa fursa hiyo ya mikopo wameanza masomo yao katika vyuo mbalimbali nchini na kwamba HESLB haijui sababu zilizowafanya wasiombe.
Kuhusu ufanisi katika utoaji wa mikopo, Mwaisobwa alisema idadi ya wanafunzi wanaoomba mikopo imeongezeka kutoka 42,729 mwaka 2005/2006 hadi kufikia wanafunzi 97,348 mwaka 2012/2013.
Aidha, Mwaisobwa alisema bajeti ya kuwakopesha wanafunzi imeongezeka kutoka Sh. bilioni 56.1 mwaka 2005/2006 hadi kufikia Sh. bilioni 306 mwaka 20012/2013.
Alisema mwaka huu serikali imeitengea bodi hiyo Sh. bilioni 325 kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi wapya, 31,647 na 62,376 wanaondelea na masomo yao katika vyuo mbalimbali.
Wakati wanafunzi hao wakikosa fursa ya mikopo, mapema mwezi huu, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, aliitaka bodi hiyo kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi na weledi mkubwa kwa mwaka huu wa masomo ili kuepusha migogoro ya wanafunzi kuhusu mikopo

Monday, June 10, 2013

TAARIFA MPYA KUTOKA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB) KWA WAOMBAJI WAKE




 
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza, Wanafunzi wanaondelea na masomo na Umma kwa ujumla kwamba mchakato wa maombi mikopo kwa mwaka wa masomo 2013/2014 ulizinduliwa rasmi tarehe 1 Mei, 2013.  Mchakato huo unaendelea vizuri na kwamba wanafunzi wengi wameweza kujaza fomu za maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao (OLAS).

2.0   WAOMBAJI WA MIKOPO WA MARA YA KWANZAUtaratibu wa kujaza fomu za maombi kwa waombaji wa mara ya kwanza, unawaelekeza waombaji hao kutoa taarifa zao za kihistoria kama vile shule za sekondari walizosoma (Kidato cha IV na Kidato cha VI), hali ya mwombaji au wazazi wake kiafya na pia taarifa za mdhamini wa mwombaji mkopo. Taarifa hizo zinaiwezesha Bodi kuchambua na kujua iwapo mwombaji



husika ana sifa ya kukopesheka au la. Ikumbukwe kwamba lengo la utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ni kuwawezesha wanafunzi wasio na uwezo wa kulipia gharama za elimu ya juu kusaidiwa kufikia malengo yao. Kwa njia ya uchambuzi huo Bodi inaweza kubaini kiasi cha mkopo unaohitajika au kiasi ambacho mwanafunzi anapaswa kuchangia katika gharama zake za elimu ya juu.

Kwa vile taarifa za ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita hazihitajiki katika hatua hii ya Mwanzo, mwombaji wa mkopo haulizwi mahali popote katika fomu yake ya maombi kuhusu kiwango cha ufaulu. Hapo baadaye Bodi itakapohitaji kuthibitisha kiwango cha ufaulu wa mwombaji itapata taarifa hizo za ufaulu moja kwa moja kutoka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).  Kutokana na utaratibu huu, mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita mwaka 2013 anaweza kuomba mkopo hata kabla ya matokeo ya Kidato cha Sita kitaifa kutolewa.  Hii ni muhimu ili kuipa Bodi muda wa kutosha kupokea maombi ya mikopo, kuchambua na kisha kupanga mikopo kwa wanafunzi stahiki watakaokuwa wamedahiliwa kwa mwaka mpya wa masomo 2013/2014.

3.0       IDADI YA WANAFUNZI WALIOKWISHAOMBA MIKOPO KUFIKIA MEI 30, 2013Hadi kufikia tarehe 30 Mei, 2013, waombaji mikopo wa mara ya kwanza waliokwishakamilisha maombi yao ni   424, Waombaji wa mara ya kwanza ambao wako kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji ni 5,320 na wanafunzi wanaoedelea na masomo waliokwishathibitisha kuendelea kupatiwa mikopo kwa mwaka ujao wa masomo ni 60,367, kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini.


4.0   HITIMISHO
Bodi inatoa msisitizo kwa waombaji wa mikopo kama ifuatavyo:

(i)      Kuzingatia taratibu zote muhimu zilizowekwa kwa ajili ya maombi ya mikopo.

(ii)     Kutumia huduma ya msaada kwa wateja (Help Desk) kikamilifu kila wanapopata tatizo lolote katika mchakato wa ujazaji wa fomu za maombi.  Huduma hiyo inapatika kwa kupiga namba 022 550 7910; kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku siku za jumatatu hadi ijumaa na kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 alasiri siku ya jumamosi.

(iii)    Kuzingatia muda uliopangwa wa maombi ya mikopo ambapo siku ya mwisho ni tarehe 30 Juni, 2013.

IMETOLEWA NA:

BODI YA WAKURUGENZI

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...