ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label Kijana aliyerusha bomu Kanisani Arusha. Show all posts
Showing posts with label Kijana aliyerusha bomu Kanisani Arusha. Show all posts

Wednesday, June 12, 2013

MTUHUMIWA WA UGAIDI WA MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA KANISANI JIJINI ARUSHA AKABIDHIWA HATI YA MSHTAKA




PictureAmbrose 
Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Devotha Kamuzora jana alimkabidhi  hati ya mashitaka yanayomkabili, Victor Ambrose (20) ambaye ni mtuhumiwa pekee aliyepandishwa kizimbani  baada ya kutokea  shambulio la bomu katika Kanisa la Mtakatifu  Joseph Mfanyakazi, Olasiti jijini Arusha.
Ambrose alikabidhiwa hati hiyo ya mashitaka yanayomkabili jana katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru jijini Arusha na kuambiwa na wakili wa Serikali, Adelaide  Kasala  kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo, haujakamilika na kumuomba Hakimu Kamuzora  kutaja tarehe nyingine.
Hakimu Kamuzora kabla ya kuahirisha kesi hiyo alimuuliza Ambrose kama alipewa hati yake dhidi ya mshitaka yanayomkabili. Ambrose alipojibu, “hapana.” Baada ya jibu hilo,


Hakimu alitoa hati hiyo na Ambrose kukabidhiwa na kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 24.Ambrose ambaye ni dereva wa bodaboda na mkazi wa Mrombo jijini Arusha, mara ya kwanza alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Arusha na baadaye kuhamishiwa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru na kusomewa mashitaka yake kwa mara ya tatu sasa huku akitakiwa kutojibu lolote, kutokana na  Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji.

Wakili wa Serikali, Adelaide Kasala  alidai mahakamani hapo Victor alitenda makosa hayo Mei 5, mwaka huu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti jijini.
 

Monday, May 13, 2013

MTUHUMIWA WA ULIPUAJI WA BOMU KATIKA KANISA OLASITI, AFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUSHOMEWA MASHTAKA 21 ARUSHA



Mtuhumiwa Bomu Kanisani Arusha, Victor Ambrose Calist (20).


MTUHUMIWA mmoja kati ya tisa waliotiwa mbaroni na jeshi la polisi baada ya kutokea mlipuko wa bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka 21 ya ma

uaji na kujaribu kuua.
Kesi ya mshtakiwa Victor Ambrose Calist (20) ambaye ni dereva wa bodaboda na mkazi wa eneo la Kwa Mromboo jijini Arushai amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu mkazi, Devotha Kamuzora.

Mtuhumiwa huyo anakabiliwa na mashtaka matatu ya mauaji ya watu watatu waliofariki dunia katika tukio ambalo lililotokea Mei 5, mwaka huu.
Mawakili wa serikali, Haruna Matagane na Zachariah Elisaria wanadai Calist pia anatuhumiwa kwa makosa 18 ya kujaribu kuua. Hata hivyo makosa mengine bado hajatajwa mpaka hivi sasa.

Pia polisi imewaachia huru raia wanne wa kigeni waliokuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika katika tukio hilo baada ya uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo kwa kushirikiana na FBI na polisi wa kimataifa (Interpol), kubaini hawakuhusika kurusha bomu katika kanisa 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...