ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label President Kikwete. Show all posts
Showing posts with label President Kikwete. Show all posts

Sunday, May 11, 2014

Rais Kikwete awatia moyo Samata na Ulimwengu huko DRC


RAIS wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete jana amewatembelea washambuliaji wawili Watanzania wanaocheza TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbwana Ally Samatta na Thomas Emannuel Ulimwengu.
Tovuti ya TPM imeandika kwamba Rais Kikwete aliwatembelea wachezaji hao leo mjini Kinshasa ambako wapo na timu yao kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya DRC dhidi ya mahasimu wao katika mbio za ubingwa AS Vita.
Rais Kikwete akiwa na Samatta kulia na Ulimwengu kushoto mjini Kinshasa jana
Rais Kikwete aliye ziarani DRC, alikuwa ameambatana na maofisa wawili wa Ubalozi wa Tanzania majira ya Saa 6:15  mchana alipokutana na wachezaji hao pamoja na Mwenyekiti  wa klabu yao, Moses Katumbi.
Rais Kikwete yupo Kinshasa tangu jana usiku kwa ziara maalum ya Saa 24 juu ya ushirikiano wa DRC na Tanzania, ambako alikutana na rais mwenzake wa huko, Joseph Kabila.
Kikwete alitumia robo saa kuzungumza na akina Samatta katika hoteli ya Congo River, ambako wameweka kambi kwa ajili ya mechi ya kukata na shoka kesho.


Rais Kikwete aliwakumbusha Samatta na Ulimwengu kwamba, Watanzania wanajivunia kuwaona wakiwa na jezi za TPM na kwamba wao ni tegemeo la timu ya taifa, Taifa Stars kwa sasa.

Thursday, November 7, 2013

HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE.

Jakaya-Kikwete_4f6c2.jpg
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ALIYOITOA BUNGENI KUHUSU JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI, 7 NOVEMBA, 2013, DODOMA
Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Mheshimiwa Mizengo Pinda, Waziri Mkuu;
Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri;
Mheshimiwa Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni;
Waheshimiwa Wabunge;
Mabibi na Mabwana;
Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kukubali ombi langu na kutenga muda wenu ili niweze kuzungumza na Wabunge wa Bunge lako Tukufu kuhusu masuala muhimu kwa uhai, ustawi na maendeleo ya nchi yetu na watu wake.
Mheshimiwa Spika;
Nimeambiwa kuwa taarifa ilipotolewa kuwa ninaomba kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wabunge, kumekuwepo na dhana mbalimbali. Wapo waliodhani kuwa nakuja kuzungumzia mchakato wa kuunda Katiba mpya na hasa matukio ya wiki chache zilizopita. Wapo waliodhani nakuja kuzungumzia "Operesheni Tokomeza". Tena wapo waliokwenda mbali na kufikiria kuwa nakuja kuwakaripia Waheshimiwa Wabunge waliotoa maoni yao kuelezea kasoro zilizojitokeza katika utekelezaji wa Operesheni hii muhimu. Na wapo pia waliodhani ninakuja kuzungumzia ushiriki wa majeshi yetu ya Tanzania katika Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa nchini Kongo.(P.T)

Tuesday, October 22, 2013

Msafara wa Rais Kikwete wazuiliwa.

MBUNGE AWACHANA MAWAZIRI MBELE YA JK , WANANCHI WAZUIA MSAFARA WA RAIS

a_7ea4a.jpg
Wananchi wa Mlangali wakiwa wamezuia msafara wa Rais Kikwete
b_80eef.jpg
Madai ya wana Ludewa kwa JK

c_2d981.jpg
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kushoto akisaidia kueleza kero za wana Ludewa kwa Rais Kikwete baada ya msafara wake kuzuiwa eneo la Mlangali leo
d_786a1.jpg
Msafara wa JK ukiwa umezuiwa eneo la Mbwila Ludewa leo
MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe awafyatua mawaziri mbele ya Rais Jakaya Kikwete kuwa wamekuwa wakitembelea jimbo lake la Ludewa wakati wa ziara ya Rais na waziri mkuu wakati siku zote wananchi wa jimbo hilo wanalia kwa kero mbali mbali.

Wednesday, July 17, 2013

Soma Taarifa Maalum Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Sudan Mheshimiwa Omar Bashir kufuatia kuuawa na kujeruhiwa kwa askari wa Tanzania, walioko katika ulinzi wa kimataifa wa amani katika jimbo la Darfur na kumtaka Rais Bashir kuchukua hatua za haraka kuwasaka na kuwakamata waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha mbele ya sheria haraka iwezekanavyo.


 Rais Jakaya Kikwete
--
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Sudan Mheshimiwa Omar Bashir kufuatia kuuawa na kujeruhiwa kwa askari wa Tanzania, walioko katika ulinzi wa kimataifa wa amani katika jimbo la Darfur na kumtaka Rais Bashir kuchukua hatua za haraka kuwasaka na kuwakamata waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha mbele ya sheria haraka iwezekanavyo.

Katika mazungumzo yao, Rais Omar Bashir amekubaliana na Rais Kikwete na kumuahidi kuwasaka  hadi kuwakamata wale wote waliohusika na kuwachukulia hatua za kisheria.

Rais Bashir amemueleza Rais Kikwete kuwa binafsi anaamini kuwa waliohusika ni wahalifu na hivyo kuahidi kuwa lazima 
watasakwa hadi kukamatwa kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

Rais Bashir amempa pole Rais Kikwete kwa tukio hilo la kusikitisha ambapo wanajeshi wa Tanzania wameenda nchini Sudan kulinda Amani na Usalama wa wananchi wa Sudan.

Mapema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Bw. Ban Ki Moon alimpigia Rais Kikwete na kumpa pole kwa mkasa huo mkubwa na wa kusikitisha ambao umewatokea wa Tanzania hao wakati wakiwa katika kutekeleza jukumu lao la kulinda amani nchini Sudan.

Hadi sasa hakuna kikundi chochote ambacho kimekiri kuhusika na shambulio hilo ingawaje kumekua na  kutupiana lawama baina ya vikundi vya kiserikali na  vya waasi katika jimbo la Darfur.

Mapigano baina ya vikundi vya kikabila na koo mbalimbali zimesababisha mapigano na uvunjifu mkubwa wa amani na usalama katika jimbo la Darfur kwa muda wa miaka 10 sasa, na mara nyingi mapigano  na tofauti zao hizo zimesababisha vifo na uvunjifu wa amani kwa wananchi wa Sudan na wageni pia.

Mwishoni mwa mwaka jana  Wanajeshi wanne kutoka Nigeria waliuawa karibu na El Geneina , Magharibi mwa Darfur ambapo pia inaelezwa na Umoja wa Mataifa kuwa wanajeshi wapatao 50 wameuawa tangu kikosi hiki cha Umoja wa Afrika kinachoundwa kwa  pamoja chini ya Umoja wa Mataifa (UNAMID) kianze operesheni yake mwishoni mwa mwaka 2007.

Taarifa za Umoja wa Mataifa pia zinaeleza kuwa kabla ya mashambulizi yaliyofanyika dhidi ya kikosi cha Tanzania jumamosi iliyopita, wanajeshi 6 wanaolinda Amani wameuawa tangu oktoba mwaka huu ambapo pia inasadikiwa kuwa watu wapatao 300,000 wameyakimbia makazi yao.

Hata hivyo kiini cha mgogoro huo unaosadikiwa kuwa ni ugomvi wa ardhi na rasilimali zilizoko katika jimbo hilo nchini Sudan.

Miili ya maaskari hao saba wa Tanzania inatarajiwa kuwasili nchini ijumaa tarehe 19, Julai kwa ajili ya maziko.
Imetolewa na:

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu
Dar-Es-Salaam, Tanzania
16 Julai, 2013

Saturday, June 29, 2013

RAIS KIKWETE AWAANDALIA MARAIS SHEREHE FUPI


 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mfalme wa Swaziland, King Mswati katika hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa kwenye viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). TBL ni moja kati kampuni zilizofadhli hafla hiyo.
 Mahali palipoandaliwa kwa dina kwenye viwanja vya Gymkhana
 Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chisano (kushoto) akikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe katika hafla ya chakula cha usiku.
 JK akiwa na Museveni wa Uganda (kushoto), King Mswati wa Swaziland na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Alnold Kilewo (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Chibuku cha Dar Brew, Kilowi Suma (wa pili kushoto), katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete  kwa marais na viongozi mbalimbali waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kutoka kulia ni Kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Halfan Mpango na Mkurugenzi wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Esther Mkwizu. Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ni kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.
 Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akihutubia katika hafla hiyo.
 Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku
 Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa marais na viongozi waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ilikuwa kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.
 Bendi ya THT ikitumbuiza katika hafla hiyo
 Msanii Mwasiti akipongezwa na Mbunge wa Afrika Mashariki, Adam Kimbisa. Kulia ni Mbunge wa bunge hilo, Shy Rose Bhanji na Abdul Mwinyi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge hilo.
                                              Kimbisa akiwa na Mwinyi, Bhanji na Richard Kasesera 
 

Saturday, June 15, 2013

President Kikwete in London for G8 Summit, meets Virgin Atlantic Founder


8E9U3186 
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his delegation in conversation with The Chairman of Virgin Group of Companies Sir. Richard Branson in London this evening. Others in the picture are from left are Minister for Transport Dr. Harrison Mwakyembe, Tanzania Tourist Board Managing Director Dr.Aloyce Nzuki, President’s advisor Economic Affairs Dr.Hamis Mwinyimvua and Tanzanian High Commissioner to the United Kingdom  Peter Kallaghe(photos by Freddy Maro)
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets and hold talks with Sir. Richard Branson in London this evening . Sir.Richard is a British  business magnate best known as the founder and chairman of Virgin Group of more than 400 companies. President Kikwete is in London UK for a three days working visit in which, among other things, he will attend the G8 summit. 8E9U3183President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets and hold talks with Sir. Richard Branson in London this evening . Sir.Richard is a British  business magnate best known as the founder and chairman of Virgin Group of more than 400 companies. President Kikwete is in London UK for a three days working visit in which, among other things, he will attend the G8 summit.

Sunday, May 26, 2013

RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA AU JIJINI ADDIS ABABA

Muono wa jicho la samaki katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013.
Viongoi mbali mbali wa nchi za Umoja wa Afrika (AU) wakiwakumbuka waliotangulia mbele ya haki.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013. 
MMarais Wastaafu wakiwa katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013.PICHA NA IKULU

Friday, May 17, 2013

Rais Barack Obama Kutembelea Tanzania Mwezi ujao



 

 President Barack Obama greets children upon his arrival to Miami International Airport in Miami, Friday, March, 4, 2011. (AP Photo/Pablo Martinez Monsivais) 



Rais Barack Obama
 
Rais Barack Obama wa Marekani anatarajia kuanza ziara yake ya pili katika bara la Afrika mwishoni wa mwezi June, ziara ambayo itamfikisha Africa ya Kusini, Tanzania na Rwanda.
Katika ziara yake hiyo, atapitia Nigeria na kuongea na rais Goodluck Jonathan pamoja na waandamizi wa serikali ya Nigeria.
 Mpango wa awali ulikuwa kwamba rais Obama angetembelea Nigeria kwa siku mbili lakini kutokana na hofu ya usalama kutoka kwa magaidi wa Boko Haram Nigeria inaonekana kwamba itashindwa kutoa ulinzi wa kutosha wa rais huyo wa Marekani hivyo atalazimika kukaa Nigeria kwa muda mchache.
Habari kutoka Ikului ya White House zinadokeza kuwa usalama utazingatiwa sana katika ziara hiyo na kama kutakuwa na sababu yeyote ya kuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Rais Obama basi ziara hiyo itakatizwa wakati wowote katika nchi ya Nigeria.
Mwaka 2009 Obama alitembelea Africa na alichagua nchi ya Ghana ambapo alikutana na Raisi (marehemu) John Atta mills, na akatoa hotuba katiba bunge la Ghana na kisha kutembelea Cape Coast Castle sehemu ambapo watumwa wa Trans Atlantic walikuwa wanapakiliwa kupelekwa Marekani wakati wa biashara ya utumwa.
Kwa sis watanzania, ziara hii ya kiongozi mkubwa duniani ina manufaa gani kibiashara, kiuchumi, kiusalama? Kuna fursa gani kwa Watanzania kama ilivyoluwa kwa Rais wa China? Ni matumaini yetu kuwa ziara hii itazidi kuliweka Taifa letu katika sura nzuri kimataifa na kitaifa. Ikumbukwe kwamba, Marais wa nchi kubwa kama Marekani wanachagua kutembelea nchi zile zinazofanya vizuri katika utawala bora, demokrasia madhubuti, uhuru wa haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari, kusimamia na kutimiza vyema malengo ya millenium..... Hivyo kwa Tanzania kupata ugeni kama huu ni ishara nzuri na chachu ya kuendelea kufanya vizuri zaidi. Mungu Ibariki Tanzania

Wednesday, May 1, 2013

Rais Jakaya Kikwete Mkoani Mbeya


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtoto mdogo muda mfupi baada ya Kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songwe mjini Mbeya jana
Maelfu ya Wakazi wa Mji wa Mbeya wakisalimiana kwa Shauku na Rais Dkt.Jakaya  Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songwe mjini Mbeya tayari kuongoza sherehe za Mei mosi zinazofanyika mkoani mbeya Leo.Picha na Freddy Maro-IKULU

Friday, April 19, 2013

President Jakaya Kikwete Sends a Condolence Message to President Obama



 President Jakaya Kikwete
--
The President of the United Republic of Tanzania, His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete has sent a condolence message to H.E. Barack Obama, President of the United States of America following the shocking news of the twin explosions, which occurred in Boston City, causing death to innocent people and severe injuries to many others.

The message reads as follows:

  “H.E. Barack Obama,
  President of the United States of America,
  Washington D.C.,
  U.S.A.

Your Excellency,
I am deeply saddened by the shocking news of the two explosions, which occurred in Boston City, causing death to innocent people and severe injuries to many others.

On behalf of the Government and People of the United Republic of Tanzania, and on my own behalf, I wish to convey my heartfelt condolences to You, and through you to the Government and the People of the United States of America, for this cowardly act.

At this moment of distress, we share your pain for the loss of life and destruction of property. We wish quick recovery to the injured. Our prayers to the families of the deceased.

Jakaya Mrisho Kikwete
PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA’’


Issued by: 


Ministry of Foreign Affairs and International Co-

operation,


Dar es Salaam.

18th April, 2013
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...