ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label habari za siasa. Show all posts
Showing posts with label habari za siasa. Show all posts

Wednesday, January 28, 2015

..Na Uwe Kondakta Wa Basi La Wanyonge...

Uwashushe abiria matajiri wachache wenye kudhamiria kuhujumu safari ya wanyonge walio wengi kwenda kujikomboa kutoka kwenye umasikini. Na matajiri hao wana hila, wanaweza hata kukuhonga kondakta wetu, kwa kwa kuwa tayari hata kukupa nauli zaidi ya uliyopanga kondakta wetu...!
Goodmorning.
Maggid.(P.T)

Tuesday, January 27, 2015

Balozi wa Jamhuri ya Korea amtembelea Waziri wa Ujenzi Ofisini kwake jijini Dar es Salaam

Displaying 1.JPG
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
kulia akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea, Chung Il kuhusiana
na mambo mbalimbali kuhusu sekta ya Ujenzi pamoja na mchakato
wa Ujenzi wa Daraja jipya litakalopita baharini pembezoni mwa daraja
la Selander.Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7.2 na uwezo wa
kupitisha magari zaidi ya 61,000 kwa siku. Ujenzi wa Daraja hilo utaanza
muda wowote kuanzia sasa. Daraja hilo litakuwa na njia nne za magari
pamoja service road njia za waenda kwa miguu kila upande.
Displaying 2.JPG
 Balozi wa Jamhuri ya Korea Chung Il akisaini kitabu cha
wageni ofisini kwa Waziri wa Ujenzi.
Displaying 3.JPG
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
kulia akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea Chung Il mara baada ya
kufanya mazungumzo ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Displaying 4.JPG
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana
jambo na Balozi huyo wa Jamhuri ya Korea Chung Il pamoja na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe na Mkurugenzi wa Barabara
Eng. Ven Ndyamukama. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-
Wizara ya Ujenzi.
                                     

Wednesday, January 21, 2015

Kauli ya Spika wa Bunge Anne Makinda kuhusu sakata la Escrow Hapo Jana



Spika wa Bunge Anne Makinda amesema sio kazi yake kuwasimamisha wenyeviti wa Kamati za Bunge ambao wanatuhumiwa na ishu ya fedha za Escrow badala yake ni wao wenyewe kujiondoa kama njia ya kutii maazimio yaliyopitishwa na Bunge ambayo yanawataka kuwajibika.
“Azimio linasema viongozi wa Kamati hizi watawajibika kwenye Kamati zao, tusibadilishe maneno. Naona na gazeti lingine linasema hawajajiuzulu, what is that? Suala la azimio kwamba viongozi hawa watatu wa Kamati wajiuzulu”—Anne Makinda

Nimetii amri ya Kinana; Asema Mwigulu


02

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mwigulu Nchemba, amekiri kupokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, inayomtaka kutoendelea na ziara zake mikoani.
Kutokana na agizo hilo, amesema ametii agizo hilo la mkuu wake wa kazi na amelitekeleza kama alivyomtaka kufanya hivyo.
Akizungumza na MTANZANIA jana ili kupata ufafanuzi wake kuhusu barua hiyo ya Kinana iliyomtaka kukatisha ziara zake kama ameipokea na anaitambua, Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, alisema agizo hilo ni halali kwa sababu ni la kiofisi, hivyo hana sababu ya kupingana nalo kwa mujibu wa utaratibu wa CCM na Serikali yake.
“Kwangu siwezi kupingana na agizo hilo halali la kiofisi, na pia ni agizo la bosi wangu ninayemsaidia kazi, na ninaamini kuna siku atanituma, na kuna siku ataniambia hiyo acha na mimi kazi yangu itakuwa utekelezaji maagizo,” alisema.
Alisema hatakuwa tayari kupinga maagizo hayo yaliyotolewa na Katibu Mkuu ambaye ni mkubwa wake wa kazi katika chama, na hivyo amesitisha ziara zake hadi pale atakaporuhusiwa.
Kauli ya Mwigulu imekuja siku moja baada ya kuripotiwa taarifa za kuandikiwa barua na Katibu Mkuu wa chama hicho, Kinana, aliyempiga marufuku kuendelea kufanya ziara ya kuzunguka katika wilaya na mikoa mbalimbali aliyokuwa akifanya kwa kutumia helikopta.
Katika barua hiyo ya Januari 18, mwaka huu ambayo ilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii, Kinana amemtaka Mwigulu kusitisha ziara zote na iwapo atataka kufanya ziara yoyote ya kichama, inambidi amuarifu na apate kibali chake.
Barua hiyo ilimlalamikia kwamba katika mikutano anayofanya amekuwa akionyesha mienendo na kauli zinazoashiria kujiandaa kugombea nafasi ya urais kupitia CCM.
Kinana alikwenda mbali na kueleza kwamba ziara za Mwigulu zimekuwa na mwelekeo wa kampeni jambo ambalo alidai ni kinyume na maadili ya chama chao.
Akizungumzia barua hiyo jana jijini Arusha, Kinana alikiri ofisi yake kumpa barua Mwigulu huku akigoma kueleza kwa undani suala hilo.
Juzi CCM kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye, ilionya hatua ya baadhi ya makada wake kuanza kampeni.
Aidha chama hicho kimewataka wapambe na wagombea wao kuacha kutoa taarifa za uzushi dhidi ya makada sita wa chama hicho kwa lengo la kupotosha umma.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari visiwani Zanzibar, Nape alisema chama hicho kitawachukulia hatua kali makada wanaogombea na wapambe wao watakaobainika kusambaza taarifa za uzushi.
Pamoja na hali hiyo, CCM imewataka wagombea hao kuwadhibiti wapambe wao na kwamba wajichunge wenyewe dhidi ya hujuma kwa chama kwani zinaweza kuwapotezea sifa za kugombea.
Nape alisema pamoja na chama kutoa tahadhari kwa baadhi ya makada wake wanaotaka kugombea urais, lakini bado wameendelea na harakati hizo.
“Pamoja na kutotolewa kwa ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama, bado zimekuwapo harakati nyingi za wanaotaka kuteuliwa na CCM kugombea nafasi mbalimbali, hasa ya urais, ambapo baadhi ni halali na nyingine haramu,” alisema Nape.

Monday, May 19, 2014

Kinana amaliza ziara Tabora kwa kishindo, maelfu wahudhuria mkutano wake wa hadhara


1. Kinana akihutubia maelfu ya watu katika Uwanja wa Stendi ya zamani mjini Tabora
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara aliofanya jana jioni kwenye Uwanja wa Stendi ya zamani mjini Tabora. Kinana amemaliza ziara yake ya siku 11 ,Mei 18, 2014.
Nape akihutubia Tabora
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo wa Tabora mjini.
2. Wasira
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, bunge wa Bunda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Steven Wassira akihutubia kwenye mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine, alieleza serikali ilivyotekeleza ilani yake ya uchaguzi hadi sasa.
3. Nkunba
Mbunge wa Sikonge, Said Mkumba kwenye mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine, ameomba sheria zianze kufuatwa kwa viongozi wa siasa kutojishirikisha na vyama vya ushirika ili kutochanganya amaslahi.
4
 Mbunge wa Viti Maalum, Ummy Mwalimu akihutubia kwenye mkutano huo na kueleza mambo mbalimbali muhimu kuhusu mchakato wa katiba mpya.
11
 Mbunge wa Jimbo Mtera, Joseph Lusinde akihutubia kwenye mkutano.
10
Matukio yakienda live kwa kupitia simu. Kulia ni Mbunge wa Nzenga, Hamis Kigwangala.
9
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, akieleza  utekelezaji wa ilani ya CCM ulivyofanywa na serikali katika huduma ya maji nchini na husuasan mkoa wa Tabora.
8
Mmoja wa Wazee waasisi wa CCM Tabora akipiga picha ya ukumbusho kwenye mkutano huo.
7
Mbunge wa Urambo, Samuel Sitta akiwasalimia wananchi kwenye mkutano huo.
6
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi alipowasili kwenye uwanja wa Stendi ya zamani ya mabasi mjini Tabora.
4 (1)
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na viongozi na msafara wake kwenda kwenye mkutano.
2
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa, wakila chakula kwa Mama Lishe wa kwenye stendi mpya ya mabasi mjini Tabora kabla ya kufanya mkutano mkubwa wa hadhara.
2
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa, wakila chakula kwa Mama Lishe wa kwenye stendi mpya ya mabasi mjini Tabora kabla ya kufanya mkutano mkubwa wa hadhara.
5.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akila chakula cha Mama lishe wa Tabora mjini stendi mpya ya mabasi kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara, Kushoto ni Mbunge wa Tabora Aden Rage na Viti Maalum Munde Tambwe. 

Sunday, May 18, 2014

TUHUMA NZITO BAJETI NISHATI NA MADINI


MUHONGO_4b051.png
Dodoma. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono wameingia katika mvutano baada ya ujumbe wa maandishi wa kutaka kukwamisha bajeti ya wizara hiyo kusambazwa kwa wabunge.

Habari za uhakika zilizopatikana jana zilieleza kuwa kiini cha mgogoro huo ni ujumbe mfupi (SMS) ambao unamtuhumu Mkono kula njama za kutaka kukwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Gazeti hili limedokezwa kuwa, SMS hiyo inadaiwa kutumwa na Waziri Muhongo kwenda kwa baadhi ya wabunge akimtuhumu Mkono kuwahonga baadhi ya wabunge Sh3 milioni kila mmoja ili kukwamisha bajeti hiyo.
Ujumbe huo unasomeka "Mhe Spika wa Bunge la Jamhuri, Sisi wabunge waadilifu tunakiri kwamba Mhe Mkono ametufuata na kutupatia fedha kila mmoja milioni 3 ili tukwamishe bajeti ya Nishati na Madini
.
Ujumbe huo umeanza pia kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwamo Jamii Forums .
Mkono
Mkono ambaye pia ni Mwanasheria mashuhuri nchini, alipoulizwa jana kama ni kweli amelalamika kwa Spika juu ya jambo hilo, alikiri na kusema alichofanya ni kulalamika kwa Spika na amemwachia alishughulikie.
"Ni kweli nimelalamika kwa Spika. Unajua taratibu za Bunge ni kuna any complaint (lalamiko) unaliwasilisha officially (rasmi) kwa Spika... hilo jambo lipo nimelifikisha kwa Spika wao ndiyo watafuatilia kwa taratibu zao,"alisema.
Profesa Muhongo
Alipotafutwa kwa njia ya simu ili alitolee ufafanuzi suala hilo, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alituma ujumbe kwa simu ukisema:
"Tutavuka tukiwa na ushindi wa maskini na wanyonge wa nchini mwetu. Tutaendelea kujenga uchumi imara utakaotoa ajira mpya na matumaini mapya kwa vijana, maskini na wanyonge wa nchini mwetu. Watanzania wamechoshwa na wizi, udalali, ubabaishaji na rushwa."
Mkurugenzi wa shughuli za Bunge, John Joel alipotafutwa jana alisema yeye hana taarifa juu ya jambo hilo akisema kama lipo, basi huenda likawa mikononi mwa Spika mwenyewe
Mvutano huo unakuja siku chache baada ya Sakata la IPTL lililoibuliwa Bungeni Ijumaa iliyopita na mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye alisema kuna ufisadi wa zaidi ya Sh200 bilioni katika akaunti ya Escrow iliyopo chini ya Benki kuu ya Tanzania (BoT).
Akaunti hiyo ilikuwa ni ya pamoja kati ya IPTL na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhifadhi malipo ya kila mwezi kwa IPTL katika kipindi chote cha mgogoro kati IPTL na Tanesco ambao uliishia mahakamani.
Tayari Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza sakata hilo.
Alhamisi wiki hii, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema aliliambia Bunge kuwa wapo watu wanaonunua mashahidi kuhusiana na sakata hilo ingawa hata hivyo hakuwataja kwa majina.
Serikali yahaha kutafuta fedha
Wakati mvutano huo ukiendelea, Serikali inahaha kutafuta fedha ili kuinusuru bajeti ya Serikali na sasa kamati ya Bunge ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake, Andrew Chenge imekuwa ikikutana na Hazina karibu kila siku.
Habari zilizopatikana jana, zilidokeza kuwa bajeti inayoiumiza kichwa zaidi ni ile ya Wizara ya Maji ambayo baadhi ya Wabunge wameapa kuikwamisha endapo Serikali haitakuja na majibu ya kuridhisha.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, Wabunge wamepania kukwamisha bajeti hiyo baada ya kugundulika kuwa wizara hiyo ilipatiwa asilimia 30 tu ya bajeti yote ya maji iliyopitishwa na Bunge mwaka jana.
Bajeti za wizara nyingine zinazoiumiza kichwa Serikali ni Wizara ya Ujenzi ambayo inasemekana inadaiwa mabilioni na makandarasi na pia baadhi ya miradi hasa ya barabara haijakamilika.
Habari zinasema Serikali inaumiza kichwa kuongeza fedha za kutoka katika Wizara hiyo ili imalize kutekeleza miradi ya barabara ikiwamo barabara zilizoahidiwa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni 2010.
"Unajua uchaguzi mkuu ni mwakani... Serikali ina kibarua kigumu cha kutekeleza miradi ya barabara na inahofu CCM itakuwa na wakati mgumu endapo kama ahadi za Rais hazitatimia,"alidokeza mbunge mmoja.
"Kwa hiyo wabunge wengi tunachachamaa kwa sababu tusipopata majibu katika Bajeti hii tumeliwa takuwa na wakati mgumu majimboni na hili hatutalikubali kabisa,"alisisitiza mbunge mmoja kutoka kanda ya Ziwa.
Kuhusu Wizara ya Maji, wabunge wanadai pamoja na kupitisha bajeti ya ya ziada ya Sh184 bilioni mwaka jana, lakini bajeti iliyokwenda kutekeleza miradi ni kati ya asilimia 30 na 40 tu.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika aliituhumu Serikali kuwa ililidanganya Bunge kwa kushindwa kuongeza Sh184 bilioni zilizotakiwa kuongezwa katika bajeti yake ya mwaka 2013/14.
Mnyika aliongeza kusema "Kati ya Sh184 bilioni, Serikali imeongeza Sh86 bilioni tu...Maana yake ni kwamba Sh98 bilioni hazijatoka mpaka sasa kwenda kwenye miradi ya jamii".
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Serikali za Mitaa (Laac), Rajabu Mmbaruk, jana aliliambia gazeti hili kuwa kwa jinsi bajeti za wizara zinavyopigwa panga, ni dhahiri Serikali inapitia wakati mgumu.
Hata hivyo, mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage, alisema inavyoonekana Serikali imekuja na mapinduzi makubwa ya bajeti kiasi kwamba haitaki tena kuwasilisha bajeti zisizotekelezeka.
"Wewe unakumbuka mwaka jana bajeti ya maji ilikwama hadi Serikali ikaongeza fedha, lakini hizo fedha zilienda zote? Na hili ndilo linaloleta shida hata kwenye bajeti ya mwaka huu,"alisema Mwijage.
Mwijage aliongeza kusema" huko nyuma Serikali ilikuwa inapitisha bajeti kuwafurahisha wabunge ili wapitishe bajeti, lakini kwa kweli nyingine hazitekelezeki na hilo limeleta mgogoro mkubwa kwa bajeti ya Maji".
Kutokana na upepo huo mbaya, Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge), William Lukuvi aliandika barua kwa Spika akiomba bajeti ya wizara hiyo isogezwe mbele.
Katika barua hiyo ambayo Lukuvi alilithibitishia gazeti hili kuiandika, alipendekeza bajeti ya Wizara ya Maji na ile ya Nishati na Madini, zote zisogezwe mbele hadi mwezi Juni badala ya kusoma mwezi huu.
"Kwa kuwa Wizara hizi bado zipo katika mazungumzo na Wizara ya Fedha kuhusu bajeti zao, ninaomba ukubali wizara hizi kubadilishiwa tarehe za kuwasilisha ili ziwasilishe mwezi Juni,"inasema barua hiyo.
Barua hiyo ya Lukuvi ya Mei 10,2014 yenye kumbukumbu 1/CEB.274/420/02 iliyotumwa kwa Spika, Anne Makinda, ilitumwa pia kwa Waziri mkuu, Waziri wa Maji na Waziri wa Nishati na Madini.
Hata hivyo, taarifa iliyopatikana jana, zinasema katika kujaribu kukokoa jahazi, kamati ya bajeti, juzi ilikutana na walipa kodi wakubwa nchini ikiwamo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kubadilishana mawazo.
Taarifa zisizo rasimi zinasema Serikali inakabiliwa na ukata mkubwa wa fedha na hiyo inasababishwa na bajeti nyingi za wizara kupunguzwa, mfano ukiwa wizara ya Mambo ya Ndani iliyopunguzwa kwa Sh500 bilioni.(E.L)
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...