Mhe.
Balozi Salome sijaona akiwapokea wajumbe waliokuwa wakihudhuria
mikutano ya IMF na WB hapa nyumbani kwake kwenye ubalozi wa Tanzani (
Tanzania House) kwa chakula cha jioni alichowaandalia.
Wajumbe
kutoka Tanzania waliohudhuria mikutano ya IMF na WB Jijini Tokyo- Japan
wakiwa katika mwaliko rasmi wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na
Mhe. Balozi Salome Sijaona katika ubalozi wa Tanzania. Kutoka kulia ni
Kamishna wa Bajeti Bi. Monica Mwamunyange, katikati ni Mhasibu Mkuu wa
Serikali Bi. Mwanaidi Mtanda na wakushoto ni Kamishna wa sera Bw.
Bedason Shallanda, wakimsikilisa kwa makini Balozi, hayupo kwenye picha.
Balozi
wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona akimkaribisha rasmi Waziri
wa Fedha pamoja na ujumbe kutoka Tanzania kwa chakula cha usiku. kutoka
kulia ni Mhe. William Mgimwa Waziri wa Fedha akifuatiwa na Waziri wa
Fedha Zanzibar Mhe. Omary Yusuph Mzee akifuatiwa na Bw.Selivicius
Likwilile Naibu Katibu Mkuu Wizara na Fedha na wengineo ni viongozi
waliohudhuria hafla hiyo Jijini Tokyo – Japan.
Wajumbe
wa mkutano wa IMF na WB wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Japan
Mhe. Salome Sijaona alipokuwa anatoa historia fupi ya ubalozi wa
Tanzania.
Wajumbe
wa mkutano wa IMF na WB wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Japan
Mhe. Salome Sijaona alipokuwa anatoa historia fupi ya ubalozi wa
Tanzania.
Balozi
wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona akimwelezea Waziri wa
fedha Mhe William Mgimwa mambo muhimu ambayo yanapaswa kufanyika katika
Balozi zetu.
Afisa wa ubalozi Bi Agnes akiwakaribisha wageni chakula cha usiku hapa ubalozini jijini Tokyo Japan.
Wajumbe kutoka Tanzania wakishiriki chakula cha jioni pamoja na Balozi Mhe. Salome sijaona.
Mhe.
William Mgimwa akimshukuru Mhe. Balozi Salome Sijaona pamoja na mme
wake Mzee Sijaona aliyekulia kwa Mhe. Balozi Salome Sijaona kwa mwaliko
wa chakula cha usiku.
Mhe.
Balozi Salome Sijaona akimweleza Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi.
Ingiahedi Mduma juu ya umuhimu wa Mawasiliano Serikalini.(Picha na Scola
Malinga).
No comments:
Post a Comment