Waziri
wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea taarifa ya kutoka kwa
Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Bw Bernard Mbakileki Wizarani Leo. Kamati hiyo
ya watu wanane iliundwa tarehe 27 Agosti 2012 kwa ajili ya kuchunguza
utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).Waziri wa Uchukuzi
ameiahidi Kamati kuwa kila kipengele walichoshauri kwenye ripoti hiyo
kitachukuliwa hatua na Mpaka Disemba mwaka huu Utekelezaji wa
Mapendekezo ya ripoti yatakuwa yametekelezwa yote.
Mwenyekiti
wa Kamati iliyoundwa kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA), Bw. Bernard Mbakileki akionyesha Magazeti mbalimbali kwa
Waziri wa Uchukuzi,Watendaji wa taasisi za Wizara Uchukuzi pamoja na
waandishi wa habari hawapo pichani yaliyokuwa yakiripoti mambo
mbalimbali wakati uchunguzi huo ulipokuwa ukiendelea.
Mwenyekiti
wa kamati ya ya uchunguzi wa utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania(TPA), Bw Bernard Mbakileki akisistiza jambo kwa Uongozi wa
Wizara ya Uchukuzi,Taasisi zilizo chini ya Wizara na waandishi wa
Habari(hawapo Pichani),wakati wa kukabidhi ripoti waliyoiandika kwa
Waziri wa Uchukuzi na kuikabidhi leo. Kulia kwa Mweyekiti wa Kamati hiyo
ni Mhe. Mhandisi. Ramo M. Makani.(Mb) ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti
wa Kamati hiyo.
Waziri
wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa waandishi wa
Habari(hawapo Pichani)baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya watu wanane
aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania(TPA).Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa mapendekezo
yalioandikwa kwenye ripoti hiyo yatafanyiwa kazi na kila aliyehusika na
ubadhilifu atachukuliwa hatua.
Waziri
wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea ripoti ya Kamati
iliyoundwa Kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)
kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw Benard Mbakileki,Kushoto kwa
Waziri Mwakyembe ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Charles
Tizeba, na Kushoto kwa Naibu Waziri huyo ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Mhandisi Omar Chambo.
No comments:
Post a Comment