Duru za jeshi la Guinea Bissau,
Afrika Magharibi, zinaeleza kuwa watu waliokuwa na silaha wameuwawa
kwenye shambulio dhidi ya kambi ya jeshi nje ya mji mkuu, Bissau.
Waandishi wa habari wanasema shambulio hilo lilofanywa usiku wa manane, litazidisha wasiwasi Guinea Bissau, ambako jeshi lilipindua serikali mwezi wa Aprili.
Fujo za mara-kwa-mara nchini Guinea Bissau zimeifanya nchi hiyo kuwa pahala pa kupitisha magendo ya mihadarati, baina ya Amerika Kusini na Ulaya.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment