Tangu kuanza
kwa mzozo wa Syria miezi kumi na minane imepita sasa, raia wengi
wameanza kujihusisha na mapigano. Mjini Aleppo, kutana na mfanyabiashara
maarufu aliyeamua kujiunga na waasi kiasi cha kuwa kamanda wao. Mateso
na dhulma alizopitia ndizo zilimfanya kujiunga na uasi
" Hatupaswi kuulizwa ikiwa tuliteswa bali ni siku gani ambayo hatujawahi kuteswa? “Daktari Abdul Raouf alikuwa mmoja wa wafanyabiashara tajiri mkubwa na maarufu sana mjini Aleppo.
Lakini wakati harakati za mapinduzi ziliposhika kasi nchini Syria, alianza kuelekeza macho yake kwenye siasa. Alianza kukutana na wengine wenye maono kama yake akitoa wito wa mageuzi.
Hapo ndipo alipokamatwa.
Nilikutana na wanachama wa vuguvugu lake la kisiri viungani mwa mji wa Aleppo wiki hii.
Nini hasa kinawapa msukumo wanaume hawa ni miezi sita ambayo walikuwa mikononi mwa majasusi wanaoogopewa sana wa kikosi cha jeshi la wanahewa.
Alielezea mateso aliyopitia ambayo yalikuwa pamoja na kuingizwa kijiti katika sehemu zake za siri.
Waasi wengine walitingisha vichwa vyao kama ishara ya kumbukumbu za waliyokumbana nayo. "Kila mtu hapa Syria anafahamu majasusi hao wanaojulikana kama “Al Khazouk ," walisema .
Kisha alisema majasusi hao walivyotumia nyaya za stima kumpiga na umeme kutoka kifuani mwake hadi katika sehemu zake za siri. Alielezea alivyochapwa kiasi cha kuvunjwa mbavu zake.
Mateso haya yanaonekana ya kuogofya na ni mbinu zile zile ambazo hutumiwa na majasusi lakini walivyokuwa wanayasimulia ni kama kitu cha kawaida.
Lakini wakati mmoja daktari alionekana kughadhabishwa sana akilia na kusema "Wallahi" yaani naapa kwa Mungu.”
Alikuwa anasimulia alivyolazimishwa kuona mfungwa mwanamke akibakwa na wanajeshiu mbele yake akiambiwa na walinzi kuwa watamfanyia vivyo hivyo mkewe ikiwa hatawapa habari wanazotaka.
Daktari Raouf alisema kuwa kabla ya kukamatwa kwao kundi lake lilikuwa limejadili ikiwa watafute fimbo za kujilinda wakati wa maandamano.
"lakini tulipoachiliwa, tuliamua kununua silaha , kila silaha ambayo tungeweza kumudu bei," alisema daktari .
Leo vuguvugu la kutetea haki za binadamu limegeuka na kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo zaidi ya watu laki tatu wameuawa kulingana na duru za upinzani.
Ghasia zimeendelea kukithiri , huku hali ikiwa mbaya zaidi katika mwezi wa Septemba. Hali ngumu imezua wanaume wenye kiu cha kufanya lolote kuokoa Syria.
Tulikuwa tumeketi mbele ya kambi moja ya waasi, wakati tu ndege ya kivita iliposikika ikipita angani. Tulijaribu kuinasa ndege hiyo kwa filamu . Lakini baadhi ya wapiganaji waliofika hapo na wao kujionea ndege hiyo walitutizama kwa shauku.
“Makundi ya kiisilamu yenye siasa kali, yanatusaidia kupigania haki yetu. Lakini nchi za Magharibi zinatutizama tu” alisema daktari Abdul Raouf. "Wewe ni nani na unatafuta nini hapa?” walihoji.
Hili kundi linashirikiana kwa karibu sana lakini halina uhusiano wa karibu na wapiganaji wengine.
Baadhi wana ndefu sana , wanavalia kanzu, wengine walionekana kuwa wageni na bila shaka hawakufurahia kuona waandishi wa kigeni .
Sio wapiganaji wa Syria peke ambao wako kwenye vita hivi. Kuna kundi moja linalojiita Jabhat al-Nusra, lenye siasa kali na ambalo inaarifiwa lina uhusiano na kundi la Al-Qaeda. Wanadai kufanya mashambulizi makubwa nchini Syria wakati vita vikikitiiri.
Hakuna takwimu za kuaminika kuhusu idadi ya wapiganaji hao, wala idadi ya wale walioingia nchini Syria kupigana.
Daktari Raouf amefanya makubaliano na wapiganaji hawa na anaamini kuwa watakubali serikali ya kidemokrasia isiyofuata misingi ya kidini na pia kusalimu silaha zao wakati vita vitakapokwisha.
Wazo hili ni vigumu kwa baadhi kuliamini.
Daktari aliondoka kwenda kuona wapiganaji wake walio katika mstari wa mbele.
Makamanda kutokla pande zote wanalengwa sana kwa mashambulizi na kile ambacho daktari Raouf hakufahamu ni kuwa mtu alikuwa anafuata gari lake.
Alitaka kumuua. Wakati alipoondoka na kuingia sehemu iliyokuwa wazi, ndege moja ya kivita ilishambulia gari lake na kumwacha na majeraha mabaya.
Nchi za Magharibi zimeamua kutowapa silaha waasi wa Syria kwa hofu ya athari zake.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment