Waziri
Kivuli wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Iringa
Mjini(CHADEMA)Mchungaji Peter MSIGWA alipozungumza na waandishi wa
habari jijini
Dar es Salaam Kuhusu kukithiri kwa uwindaji haramu wa wanyama pori
licha ya serikali kubadilisha Waziri Wa maliasili na Utalii,Kulia ni
Mbunge wa Mbeyea Mjini(CHADEMA)Joseph Mbilinyi.Picha na Michael Jamson
--
WAZIRI
Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msingwa amemtaka Rais
Jakaya Kikwete kumchukulia hatua kali za nidhamu Waziri wa wizara hiyo,
Balozi Khamis Kagashehi kutokana na kuonyesha udhaifu kiutendaji.
Hatua hiyo inatokana na taarifa za kukamatwa kwa kontena mbili za pembe za ndovu zenye thamani ya Sh5.4 bilioni.
Pembe hizo zilikamatwa na maofisa forodha wa Hong Kong zilizokuwa zikisafirishwa kutoka Tanzania na Kenya.
Pembe hizo
zilikuwa vipande 1,209 vyenye uzito wa tani nne zilikamatwa wiki
iliyopita nchini China, zikiwa kwenye kontena mbili ambazo ziliwekwa
alama kuwa zimebeba plastiki chakavu na maharage aina ya Roscoco.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Mchungaji Msigwa alisema ufisadi wa kusafirisha
Twiga nje ya nchi hadi kwenye wizi wa pembe za ndovu, ni mwendelezo wa
kutokuwapo kwa ufanisi katika wizara hiyo.
Alisema
tangu kutokea kwa taarifa hizo za kukamatwa kwa pembe za ndovu Waziri
ameshindwa kuueleza umma wa watanzania kuhusu hatua ambayo ameichukua
akiwa kama mtendaji mkuu wa wizara.
“Katika
bunge la bajeti nilitoa rai, nikimtaka Waziri Kagasheki na Serikali
kuchukua hatua kuokoa maliasili na utajiri huu wa taifa, lakini hakuna
kinachoendelea,” alisema Mchungaji Msingwa.
“Uwendawazimu
ni kufanya jambo lilelile kwa njia ileile huku ukitegemea matokeo
tofauti, hivyo umefika wakati kwa Rais Kikwete kumchukulia hatua Waziri
Kagasheki,” alisema.
Alisema serikali imewachukulia hatua kali viongozi wadogo na kuwaacha majangili wakubwa wakiendeleza wimbi la kuihujumu rasilimali ya Watanzania.
Alisema serikali imewachukulia hatua kali viongozi wadogo na kuwaacha majangili wakubwa wakiendeleza wimbi la kuihujumu rasilimali ya Watanzania.
“Tukumbuke
Mwalimu (Julius) Nyerere aliwahi kusema serikali ‘Currupt’ hukimbizana
na watu wadogowadogo tu, Serikali ‘corrupt’ haiwezi kuwachukulia hatua
watoa rushwa wakubwa,” alisema Mchungaji Msingwa.
Jitihada za
kumpata Balozi Kagasheki kuzungumzia suala hilo jana, hazikufanikiwa
kutokana na simu yake ya mkononi kutokuwa hewani muda wote.
No comments:
Post a Comment