Ndege zikiwa zimetulia baada ya safari zote za aga kusitishwa
Treni ba mabasi ya abiria yasimamisha huduma kwa muda
Abiria wauchapa usingizi baada ya safari za ndege zao kusitishwa
Magari yaliyoangukiwa na miti
Mojawapo
ya vimbunga vikubwa zaidi kuwahi kupiga Mashariki mwa Pwani ya Marekani
kimesababisha mafuriko makubwa katika baadhi ya sehemu za mji wa New
York.
Maeneo mengi mjini yamewachwa katika giza baada ya huduma za umeme kukatizwa.Dhoruba kali kutoka mjini Florida hadi nchini Canada imepiga Mashariki mwa Marekani na kusababisha mawimbi makali mjini New York.
Maji yamefurika kwenye barabara na katika njia za reli pamoja, maeneo ya kuegesha magari na katika eneo la Ground Zero, eneo ambalo mashambulizi ya Septemba kumi na moja yalitokea.
Sehemu kubwa za mji wa New York ziko kwenye giza baada ya milingoti ya umeme kuharibiwa.
Wagonjwa waliondolewa kwenye hospitali moja baada ya umeme kukatika.
Zaidi ya watu milioni tano walisemekana kukosa umeme katika eneo la Pwani baada dhoruba kali huku takriban wengine milioni moja wakishauriwa kuhama nyumba zao.
No comments:
Post a Comment