Mjumbe kutoka mkoa wa Mwanza, akipiga kura kuchagua Mwenyekiti, wakati wa Mkutano Mkuu wa UVCCM mjini Dodoma.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akicharaza gita zito la besi na
bendi ya Vijana Jazz wakati wa Mkutano Mkuu wa nane wa UVCCM kwenye
Ukumbi wa Mwalimu Nyerere mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela akitoa utaratibu kabla ya kuanza uchaguzi mkuu wa jumuia hiyo leo mjini Dodoma.
Shamrashamra za Vijana kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere katika mkutano wa nane wa UVCCM mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua mkutano Mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM mjini Dodoma leo.
Wagombea
waliokuwa wanawania nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM. Kutoka kushoto, Lulu
Abdallah Mshamu ambaye alijitoa wakati akijieleza kwa wajumbe,Khamis
Sadifa Juma na Msaraka Rashid Simai ambao ndio waliochuana.
-Wajumbe ukumbini wamwita ‘jembe’
- Anogesha mkutano kwa kucharaza gita na Vijana Jazz
NA MWANDISHI WETU
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, amenogesha
Mkutano mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM, UVCCM unaoendea mjini
Dodoma.
Licha
ya viongozi wengi kushangiliwa wakati wa kuingia ukumbini, nderemo na
shamaramshamra zililipuka zaidi kutoka kwa wajumbe wa Mkutano huo wakati
Nape alipotangazwa kuwasili.
“Jembe,
jembe, jembe”, wajumbe walisikika wakilipuka na kumshangilia baada ya
Mkuu wa Umahasishaji na Chipukizi wa UVCCM, Esther Bulaya alipotangaza
kuwasili kwa Nape ukumbini.
Ukumbi
ulilipuka zaidi Nape alipopanda jukwaani na kuliungurumisha gita zito
la besi, wakati Bendi ya Vijana Jazz ilipokuwa ikitumbuiza wimbo maalum,
baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuwasili ukumbini.
Viongozi
wengine walioonyesha kuwakuna wajumbe wa mkutano huo wa vijana ambao ni
wa Uchaguzi Mkuu ni pamoja, na Mbunge wa Bumbuli Januari Makamba,
Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC
Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma.
Baada
ya mkutano kufunguliwa na Rais Kikwete, uchaguzi uliendelea ambapo leo,
wanatarajiwa kupatika viongozi wapya wa UVCCM ngazi ya Mwenyekiti,
Makamu Mwenyekiti na Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Ujumbe wa
Baraza Kuu UVCCM na wawakilishi kwenye jumuia zingine.
Katika
nafasi ya Uwenyekiti ushindani ulihamia kwa wagombea wawili Msaraka
Rashid Simai, Khamis Sadifa Juma baada ya mgombea mwingine Abdallah Lulu
Mshamu kujitoa wakati wa kujieleza kwa wajumbe ukumbini.
Nafasi
ya Makamu Mwenyekiti wamechuana Ally Salum Hapi, Paul Christian Makonda
Mboni Mohamed Mhita wakati nafasi zingine ni, Halmashauri Kuu ya Taifa
Viti sita (Bara) wagombea 40, Viti Vinne (Zanzibar) wagombea 22, Nafasi
ya Baraza Kuu la Vijana Taifa Viti vitano Bara wagombea 39 na viti
vitano Zanzibar wagombea 14, Uwakilishi Wazazi Taifa na Jumuia ya
Wanawake Tanzania (UWT) wagombea 16 kila nafasi.
No comments:
Post a Comment