Afisa
Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR)
Bw. Austin Makani akizungumza na wakazi wa kata ya Pugu akizungumzia
kwanini Umoja wa Mataifa katika wiki hii ya maadhimisho ya miaka 67
tangu kuanzishwa pamoja na mambo mengine imeamua kutilia mkazo suala la
Utunzaji wa Mazingira kwa kuwa ni moja ya maeneo muhimu unapozungumzia
suala zima la kutoa elimu juu ya mabadiliko ya Tabia nchi.
Mtaalamu
wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro (wa pili kulia)
aliyemwakilisha mgeni rasni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,
Bi. Stella Karegesya UNV Program Officer Tanzania (kulia) Mwenyekiti wa
Mtaa wa Kigogo Fresh Bw. Ally Maguno, Afisa Mtendaji wa Kata ya Pugu Bw.
Justin Nyangwe na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kinyamwezi Bw. Mohamedi Abdalah
aliyemwakilisha Diwani wa Kata ya Pugu katika meza kuu.
Afisa
Mtendaji wa Kata ya Pugu Bw. Justin Nyangwe akizungumza wakati wa
kumkaribisha mgeni rasmi ambapo ametoa shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa
kuwapa umuhimu wakazi wa Pugu kwa kuchukua hatua ya kushirikiana nao
katika suala zima la kuboresha mazingira na wanaahidi kuwa mfano wa
kuigwa katika utunzaji wa mazingira.
Mtaalamu
wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro (wa pili kulia)
aliyemwakilisha mgeni rasni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini
akitoa nasaha zake katika wiki ya maamdhisho ya Umoja wa Mataifa ambapo
Umoja huo ulikwenda kufanya kampeni ya kuhimiza wananchi kutunza
mazingira katika Kata ya Pugu,
Akizungumza
na wakazi hao amewataka kujenga utamaduni wa kupanda miti ikiwa ni
pamoja kutunza msitu uliopo katika eneo hilo ambao kwa sasa unaonekana
kunyauka na hata kufikia kukimbiwa na wanyama na ndege asili jambo
alilosema iwapo hazitachukuliwa hatua za makusudi kuutunza msitu huo
utatoweka na kuwa mfano mbaya kwa vizazi vijavyo.
Aidha
amesema upo umuhimu wa miradi ya upandaji miti kuwashirikisha zaidi
wakazi wa eneo husika na kutaka kampeni kama hizo zishirikishe Tume ya
Taifa ya Kuhifadhi Mazingira ili kuweza kutekeleza mikakati ya kutoa
elimu juu ya mabadiliko ya tabia nchi kwa ufanisi zaidi.
Muasisi
na Mkurugenzi wa Young Tanzanian For Community Prosperity (YTCP) Bw.
Alfred Magahema akisalisha mada juu ya umuhimu na njia bora za kutoa
elimu kwa Watnzania juu ya mabadiliko ya Tabia nchi ambapo ameshauri
elimu hiyo isitolewe mijini tu bali hata katika maeneo yaliyoko nje ya
mji pamoja na Vijijini na kuwataka wale wote walioelewa somo hilo wakawe
walimu na wahamasishaji kwa wenzao kwa kuwaelekeza umuhimu wa utunzaji
Mazangira.
Vijana
wa Tanzania waliojitolea kwa maendeleo ya Jamii wa Taasisi ya YTCP
wakiwa katika makundi na wananchi wa Kata ya Pugu kujadili majumuisho ya
nini Kifanyike, njia gani zitumike katika kuboresha mazingira ili
kukabiliana na tabia ya nchi kwa manufaa ya Taifa wakati maadhimisho ya
wiki ya Umoja wa Mataifa yenye Kauli mbiu ”BORESHA MAZINGIRA KWA MAISHA
ENDELEVU”.
Jovine
Malago wa YTCP (kulia) na wakazi wa Pugu wakiwasalishi mapendekezo
waliyokubaliana baada ya kufanya majadiliano katika makundi kuhusiana na
zipi njia bora zitakazowezesha kuwashirikisha wananchi katika utunzaji
wa Mazingira.
Pichani
Juu na Chini ni wakazi wa Kata ya Pugu wakifuatilia mafunzo mafupi ya
namna ya utunzaji Mazingira kutoka kwa Vijana wa YTCP wakati wa wiki ya
Umoja wa Mataifa ambapo ulikwenda kuhamasisha kampeni ya utunzaji
mazingira na umuhimu wa kupanda miti.
Afisa
Maendeleo ya Jamii kata ya Pugu Bw. Mlagala akitoa malalamiko ambapo
amelizungumzia dampo la Pugu limeathiri wakazi wa eneo hilo ikiwa ni
pamoja na kusababisha magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu na pia
amezingumzia suala la kukithiri kwa umaskini wa kipato na fikra
kuhusiana na utunzaji wa Mazingira na kuuomba Umoja wa Mataifa kupitia
miradi yake ya Maendeleo uwasaidie kuwawezesha kuondokana na umaskini
kupitia miradi ya ufugaji wa Nyuki na kilimo cha Uyoga.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Kinyamwezi Bw. Mohammed Abdalah (kushoto) akimwongoza
Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro (katikati)
kuelekea sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kupanda miti sambamba
na wanakijiji wa kata ya Pugu.
Pichani
Juu na Chini ni Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani
Ngusaro akipanda mti kwa ajili ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira
ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa katika kusheherekea
miaka 67 tangu kuanza kwa shirika hilo yenye kauli mbiu “BORESHA
MAZINGIRA KWA MAISHA ENDELEVU”.
Pichani
Juu na Chini ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kinyamwezi Kata ya Pugu Bw.
Mohamedi Abdalah akipanda mti kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa
katika kutunza mazingira wakati wa maadhimisho ya wiki ya Umoja wa
Mataifa nchini Tanzania.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Pugu Bw. Justin Nyangwe akishiriki zoezi la upandaji miti.
Wakazi
wa kata ya Pugu katika Picha ya Pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa
Mataifa na vijana wakujitolea wa YTCP baada ya kukamilika kwa zoezi la
upandaji miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa
kusheherekea miaka 67.
No comments:
Post a Comment