Waziri Mkuu wa Finland Bw. Jyrki Katainen.
 
Walinzi wa Usalama nchini Finland wamefanikiwa  kumzuia mtu aliekuwa na kisu wakati alipokuwa anamsogelea Waziri Mkuu Jyrki Katainen.
Waziri Mkuu huyo alikuwa anawahutubia watu kwenye  mkutano wa hadhara kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mtu anaekadiriwa kuwa katika umri wa miaka ya 30 alijitokeza na kusalimiana na waziri Mkuu huyo.Lakini baadae walinzi waliona kuwa alikuwa na kisu mkononi na ndipo walipomwondolea mbali.
Msemaji wa serikali ameeleza kuwa Waziri Mkuu  Katainen hakudhurika na aliendelea na kazi kama kawaida.