Picha mbali mbali za mizoga ya faru ambao ambao wameuwawa kwa sumu na kuondolewa pembe
Kitoto cha faru kikiwa hakijui la kufanya baada ya mama yake kuuwawa na maharamia kwa ajili ya pembe
Bango likimwonyesha haramia Chumlong Lemtongthai raiya wa Thailand aliyehukumiwa miaka 40 kwa kuua faru
Haramia Chumlong Lemtongthai akiwa mahakamani Afrika Kusini
baadhi ya pembe za faru zilizokamatwa
Haramia Chumlong Lemtongthai akiwa mahakamani na mawakili wake
Haramia Chumlong Lemtongthai akijitetea mahakamani
Mahakama nchini Afrika
Kusini imemhukumu kifungo cha miaka arobaini raia mmoja wa Thailand
aliyepatikana na hatia ya kuuza pembe za vifaru na kuandaa maonyesho ya
uwindaji yasiyokubalika
Chumlong Lemtongthai alikiri kosa la kuwalipa makahaba kuweza kufanya maonyesho ya uwindaji wa vifaru.Pembe hizo ziliuzwa barani Asia ambako soko la pembe hizi ni kubwa sana kwani hutumiwa kama dawa.
Zaidi ya vifaru miatano wameuawa nchini humo na wawindaji haramu mwaka huu pekee.
Akitoa hukumu hiyo jaji alisema kuwa hataki wajukuu wake wakuwe bila kujionea vifaru nchii humo.
Tanzania bado tunapiga bla bla tu kwenye hili. Tunatakiwa kuiga mfano wa Afrika Kusini katika kukabiliana na uharamia katika mbuga zetu. Tunasikia tu watu wanakamatwa lakini hawatajwi kwa majina hata kusikia wamepewa hukumu kali kama fundisho. Tuige mfano wa Afriak Kusini kuwaonyesha hadharani ili wajukuu wetu wajue kuwa Tanzania haina faru tena kutokana na uharamia wa fulani bin fulani.
No comments:
Post a Comment