Spika
wa Bunge Anne Makinda akisoma taarifa Bungeni mjini Dodoma leo juu ya
ripoti ya tuhumu za rushwa zilizowakabili wabunge kadhaa.
Wabunge
waliotuhumiwa kwa kujihusisha na rushwa leo wamesafishwa na Spika Anne
Makinda baada ya kutoa ripoti aliyosoma leo iliyoshindwakudhibitisha
kuwa wabunge hao walikuwa wamekula rushwa. Kutokana na ripoti hiyo imemlazimu Spika kukemea tabia ya baadhi ya
wabunge kuwatuhumu watu au wabunge wengine juu ya rushwa wakati
wakichangia hoja bungeni.
Akitoa uamuzi wake Spika Anna Makinda alimewapa onyo wabunge waliotoa matamko ya rushwa wakiwa wakichangia hoja bungeni. Spika pia amewapa onyo kali Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini,
Eliakimu Maswi na Waziri wa wizara hiyo, Profesa Soppter Muhongo kwa
kuwazushia tuhuma za rushwa wabunge kadhaa. Spika Anna makinda amelaumu tabia hiyo ya kuwatuhumu wabunge kuhusiana na Rushwa. Baadhi ya wabunge hao walitajwa na ripoti ya Spika Anna Makinda kwamba
wamejihusisha na rushwa ni pamoja na wabunge wa Viti Maalum, Saraha
Msafiri Ali na Munde Tambwe. Wengine ni Mbunge wa Bukene (CCM), Selemani Zedi , Mbunge wa
Simanjiro (CCM) , Christopher Ole-Sendeka na Zitto Kabwe wa Kigoma
Kaskazini (CHADEMA).
Mbunge
Sarah Msafiri (wa kwanza kushoto) aliyetuhumiiwa kuomba rushwa ya Sh
Milioni 50 kutoka kwa Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini
Eliakim Maswi, akiwa bungeni na wenzake wakati ripoti ya Spika akisoma
leo bungeni.
JAMHURI
YA
MUUNGANO
WA
TANZANIA
BUNGE
LA
TANZANIA
Tel: +255 22
21122065/7Fax No. +255 22 2112538Email: tanzparl@parliament.go.tz Ofisi
ya BungeS.L.P. 941
DODOMA
____________ UAMUZI
WA SPIKAKUHUSU:TUHUMA KWAMBA BAADHI YA WABUNGE NA WAJUMBE WA KAMATI YA
NISHATINA MADINI WALIJIHUSISHA NA VITENDO VYA RUSHWA KATIKA KUTEKELEZA KAZIZAO
ZA KIBUNGE ___________ Umetolewa na Mhe. Anne S. Makinda
(MB.)SPIKAUAMUZI WA SPIKA KUHUSU TUHUMA KWAMBA BAADHI YA WABUNGE NAWAJUMBE WA
KAMATI YA NISHATI NA MADINI WALIJIHUSISHA NA VITENDO VYARUSHWA KATIKA
KUTEKELEZA KAZI ZAO ZA KIBUNGE
[Chini ya
Kanuni ya 5(1) na 72(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007,na Kifungu
cha 12(1), (2)na 25(c) cha Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki zaBunge, Sura ya
296]
________________
SEHEMU YA
KWANZAMaelezo ya Utangulizi
Waheshimiwa
Wabunge, mtakumbuka kwamba, tarehe 27 na 28 Julai, 2012wakati wa mjadala
waHotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, baadhiya Wabunge walitoa
michango mbalimbali na kuibua tuhuma zilizotolewa piakwa maandishi, kwa barua
ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw.Eliakim C. Maswi, kwa Katibu
wa Bunge kama ifuatavyo:-
Kwamba,
baadhi ya Wabunge na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bungeya Nishati na Madini
walikuwa wanaenda Ofisini kwa Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini kuomba
rushwa ili waitetee Wizara hiyo inapowasilisha taarifambalimbali kwenye Kamati
hiyo;Kwamba, baadhi ya Wabunge na Wajumbe wa Kamati hiyo wana mgonganowa kimaslahi
(conflict of interest) katika kutekeleza majukumu yao ya kibungeya kuisimamia
Wizara ya Nishati na Madini, kwa kufanya biashara na Shirika laUsambazi wa
Umeme (TANESCO);Kwamba, baadhi ya Wabunge wamekuwa wanajihusisha na vitendo
vyarushwa kwa kupokea fedha kutoka kwenye Makampuni ya mafuta, kwa lengola
kuyatetea Makampuni hayo kwa kupinga uamuzi wa Katibu Mkuu wa Wizaraya Nishati
na Madini, Bw. Eliakim C. Maswi wa kutoa Zabuni ya Ununuzi wamafuta mazito ya
kuendeshea mitambo ya IPTL kwa Kampuni ya PUMA Energy(T) Ltd;Kwamba, kutokana
na kupewa rushwa na baadhi ya Makampuni ya mafuta iliwayatetee, baadhi ya
Wabunge walikuwa wanaendesha kampeni yakukwamisha kupitishwa kwa Bajeti ya
Wizara ya Nishati na Madini, kwa mwakawa Fedha 2012/2013.Wakati wa mjadala huo,
Mheshimiwa Vita Rashid Mfaume Kawawa (MB.) alitoahoja kwa mujibu wa Kanuni ya
5(1), 53(2) na 55(3) (f) ya Kanuni za Kudumu zaBunge, Toleo la 2007 kwamba, kwa
kuzingatia kuwamichango mingi iliyotolewana Wabunge wakati wa kuchangia Hotuba
hiyo imewatuhumu baadhi yaWabunge na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na
Madini kujihusisha navitendo vya rushwa, anaomba mambo yafutayo yafanyike:-
Kamati ya
Bunge na Nishati na Madini ivunjwe; na
Tuhuma za
vitendo vya rushwa zilizotolewa zifanyiwe uchunguzi na Kamati yaHaki, Maadili
na Madaraka ya Bunge.Baada ya Mheshimiwa Vita Rashid Mfaume Kawawa kuwasilisha
hoja yake,Bunge lilipitisha Azimio kwamba, “Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati naMadini ivunjwe; na pia kwamba, tuhuma za vitendo vya rushwa
zilizotolewazichunguzwe na Kamati Ndogoya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge
nakumshauri Spika.”Katika kutekeleza Azimio hilo la Bunge, niliivunja Kamati ya
Bunge ya Nishati naMadini, kwa kutoa tamko la kufanya hivyo Bungeni, kwa
mamlaka niliyonayo
kwa mujibu
wa Kanuni ya 113(3), ikisomwa pamoja na Kifungu cha 48(1) (a) chaSheria ya
Tafsiri za Sheria, Sura ya 1 [The Interpretation of Laws Act (Cap.1)].Aidha,
kwa kuzingatia kuwa kwa hali-asili yake, jambo hilo linahusu ‘haki zaBunge’
(Parliamentary privilege), nililipeleka kwenye Kamati Ndogo ya Haki,Maadili na
Madaraka ya Bunge ili Kamati hiyo ilifanyie uchunguzi na kunishauri.Kamati hiyo
Ndogo ilipewa Hadidu ya Rejea moja tu, ambayo ni:“Kuchunguzana kumshauri Spika
iwapo tuhuma kwabaadhi ya Wabunge na Wajumbe waKamati yaNishati na
Madinikujihusisha na vitendo vya rushwa ni za kweli auhapana.”Baada ya Kamati
hiyo kukamilisha kazi yake, iliwasilisha taarifayake rasmikwangu ili kwa wakati
muafaka,niweze kutoa Uamuzi wa Spika kuhusu sualahilo.Kwa kuzingatia kuwa suala
hilo linahusu “haki za Bunge,” (parliamentaryprivilege),napenda nitoemaelezo ya
ufafanuzi kuhusu dhana hiyo kabla yakutoa Uamuzi wa Spika.
Dhana ya
Haki za Bunge (Parliamentary Privilege) na Madhumuni yake
Kwa ajili ya
Uendeshaji bora wa shughuli zake, Bunge kwa mujibu wa Katiba naSheria, limepewa
kinga,madaraka na haki, fulani (immunities, powers andprivileges) ambazo
zinaliwezesha kutekeleza majukumu yake kwa niaba yawananchi, kwa uhuru, uwazi
na uwajibikaji, bila ya kuingiliwa au kutishwa namtu au chombo chochote cha
Dola.Katika Kitabu chake kiitwacho “Treaties on the Law, Privileges,
Proceedings andUsage of Parliament,1Erskine Mayametoa tafsiri ya ‘haki za
Bunge’ kamaifuatavyo:“Parliamentary privilege is the sum of the peculiar rights
enjoyed by the Housecollectively… and by Members of the House individually,
without which theycould not discharge their functions”2Kwa tafsiri, nukuu hiyo
inaeleza kwamba, “maana ya haki za Bunge ni haki zoteza kipekee za Bunge na za
kila Mbunge binafsi kwa ujumla wake, ambazo bilakuwepo kwake, Bunge na Wabunge
hawawezi kutekeleza majukumu yao.”Mwandishi mwingine aitwae Hood Phillips3
ameeleza kwamba, kila Bungelinatekeleza madaraka na haki ambazo zinachukuliwa
kuwa ni muhimu kwahadhi ya Bunge, na pia katika kuliwezesha Bunge kutekeleza
majukumu yake.Kwa ajili ya ufasaha zaidi, maelezo ya Mwandishi huyo kwa lugha
aliyoitumiayanasomeka kama ifuatavyo:-
“Each House
exercises certain powers and privileges which are regarded asessential to the
dignity and proper functioning of Parliament.”
Ufafanuzi
huo unaonyesha kwamba, madhumuni ya msingi ya kuwepo kwa‘haki za Bunge’ ni
kuliwezesha Bunge na Wabunge kutekeleza ipasavyomajukumu yao ya
kikatiba.Erskine May ameelezea kuhusu madhumuni ya uwepo wa ‘haki za Bunge’
kamaifuatavyo:-
“… certain
rights and immunities such as freedom from arrest or freedom
of speech belong primarily to individual Members of the House and
exist becausethe House cannot perform its functions without the unimpeded use
of the services of its Members. Other such rights and immunities, such as
the power topunish for contempt and breach and the power to regulate its own
constitutionbelong primarily to the House as a collective body, for the protection
of itsmembers and the vindication of its own authority and dignity. … The
term“privilege” is therefore used to mean those fundamental rights
absolutelynecessary for the exercise and due execution of constitutional powers
andfunctions of the House.”4
Maelezo hayo
yanaonyesha kwamba, uwepo wa ‘haki za Bunge’ ni nyezomuhimu kwa ajili ya
kulinda hadhi na heshima ya Bunge, na pia kwa ajili yakuliwezesha Bunge
kutekeleza majukumu yake ya kikatiba ipasavyo. Maelezohayo yanaonyesha pia
kwamba, haki hizo zinawalinda na kuwawezeshaWabunge kutekeleza majukumu yao ya
kibunge ndani ya Bunge na Kamatizake, kwa uhuru, uadilifu na bila woga wa
vitisho vya namna yoyoteile, kutokakatika Mihimili ya Dola, au vyombo vingine
vya Dola au watu binafsi.Mwaka 1873, Mbunge mmoja wa Bunge la Canada alieleza
kuhusu ‘haki zaBunge’ katika maneno yafuatayo:-“The privileges of Parliament
are the privileges of the people, and the rights ofParliament are the rights of
the people.”Kwa lugha ya Kiswahili, nukuu hiyo inaeleza kwamba, “Kinga za Bunge
ni kingaza wananchi, na haki za Bunge ni haki za wananchi.” Kwa maneno
mengine,‘haki za Bunge’ hutumiwa na Bunge na Wabunge, kwa niaba ya
wananchiwanaowawakilisha (i.e. Privileges are enjoyed by the House and by it
Memberson behalf of the citizens whom they represent).Kwa nchi yetu ya
Tanzania, msingi wa ‘haki za Bunge’ letu ni Ibara ya 100 yaKatiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, 1977 inayoelekeza kwamba:-
No comments:
Post a Comment