Godbless Lema akiwasili katika viwanja vya Mahakama ya Kuu jijini Dar leo.
Wapenzi wa Chadema wakimlaki Mhe. Lema mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama leo.
Jopo la Majaji likiwa tayari kuanza kazi.
Kutoka kushoto, Henry Kileo, Nuru Ndosi na Mhe. Godbless Lema wakiwa mahakamani leo.
Henry Kileo akiwa ndani ya ukumbi wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam.
Katibu
wa Chadema Kanda ya Kinondoni, Henry Kileo (kushoto) akibadilishana
mawazo na mdau wa Chadema mara baada ya kuwasili viwanja vya Mahakama
Kuu leo. Habari / Picha kwa hisani ya ARUSHA255
--
Pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufani kupitia Wakili wao
Alute Mughwai ili rufaa ya Lema kupinga kuvuliwa ubunge isisikilizwe
limetupiliwa mbali na Mahakama baada ya kuridhika kwamba kosoro
zilizolalamikiwa zilikuwa kwa upande wa Mahakama.
Pia kifungu
kilichomhukumu Lema kina makosa hivyo kesi itatajwa tena baada ya siku
14 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza hoja za waliokata rufaa. Mawakili
wa Mhe. Godbless Lema wanahitajika kutimiza mahitaji fulani ya kisheria
ndani ya siku 14 ili shauri la rufaa hiyo iweze kupangiwa siku ya
kusikilizwa na kuamuliwa.
Wadaiwa kwenye shauri hilo ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi. Lema anawakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu.

No comments:
Post a Comment