Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akijibu maswali ya papo kwa hapo ya wabunge katika
kikao cha bunge mjini Dodoma leo asubuhi na kudai kuwa katiba mpya
itakamilika 2014.
Kiongozi wa kambi ya Upinzani bungeni Freeman Mbowe akimuuliza swali Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Na.Mwandishi wetu, Dodoma.
Bunge
leo limeambiwa kuwa Katiba mpya itakuwa tayari ifikapo mwaka 2014 na
Tanzania itafanya uchaguzi wake wa kwanza mwaka 2015 kwa kutumia katiba
mpya.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa akijibu maswali ya wabunge katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo bungeni leo.
Akimjibu
bungeni Kiongozi wa kambi ya upinzani Mh. Freeman Mbowe aliyetaka kujua
kuwa ni lini sheria zinazotawala daftari la kupiga kura zitarekebishwa
ili kuwapa fursa kubwa wapiga kura.
Pinda
amesema kuwa marekebisho ya sheria hizo ni moja ya masuala
yanayoratibiwa na tume ya jaji Joseph Warioba ya kukusanya maoni ya
kuunda katiba mpya ya Tanzania.
Waziri
Mkuu ameliambia bunge kuwa kwa mujibu wa Jaji Warioba katiba mpya
inayotarajiwa kuwa na marekebisho mapya mengi ikiwemo ya sheria za
uchaguzi itakamilika kama ilivyopangwa.
No comments:
Post a Comment