HIVI NDIVYO ALIVYOUNGUZWA MTOTO ANETH NA MAMA YAKE
MDOGO
HUYU NDIYO MAMA MDOGO WA ANETH AMEJULIKANA KWA JINA LA
BAHATI LUKANGARA NDIYO ALIYEMUUNGUZA MTOTO
ANETH
HAPA MAJIRANI WAKIJARIBU KUMUULIZA SABABU ZA KUMUUNGUZA
HUYO MALAIKA WA MUNGU NINI SABABU YAKE MPAKA AKACHUKUA HATUA YA KUMUUNGUZA
LAKINI KWA KIBURI CHA HUYO MAMA ALIKAA KIMYA KABISA BILA YA KUJIBU
CHOCHOTE
WANANCHI WENYE HASIRA KALI WALIMCHUKUA MAMA HUYO NA
KUMPELEKA KITUO CHA POLISI
MWENYEKITI WA MTAA HUO HABIBA MWAKITALU AMEMBEBA MTOTO
ANETH TAYARI KWA KUMPELEKA HOSPITALI HUKU NYUMA AKIFUATIWA NA MWESHIMIWA DIWANI
KATA YA MAJENGO SAMWELI
MTUHUMIWA NA MGONJWA WANAINGIZWA KATIKA GARI LA
MWESHIMIWA DIWANI TAYARI KWA KUPELEKWA POLISI PICHA KWA
HISANI YA KALULUNGA ,HABARI KWA
HISANI YA EMANUEL MADAFA
---
Katika hali isiyo ya Kawaida Mkazi wa majengo jijini Mbeya Ndugu
Bahati Rukangara amemchoma moto mtoto mdogo wa mika 3 aliyefahamika kwa jina la
Aneth kisha kumfungia Ndani na kumlazimisha ale kinyessi chake.
Akizungumza Mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Habiba Mwakitabu
amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10 :30 asabuhi ambapo majirani
na mwanamke huyo waligundua mara baada ya kusikia sauti ya mtoto huyo akilia
kutokana na maumivu.
Amesema mara baada ya kusikia sauti hiyo walifika eno hilo na
kunza kumhoji ili kufahamu kiini cha tatizo hilo ambapo alishindwa kutoa
ushirikiano ndipo walipo anza kumpiga .
Amesema kutokana na hali hiyo majirani walilazimika kubomoa
mlango ndipo walipo mkuta mtoto huyo akiwa uchi huku ameungua vibaya mwilini
hasa katika upande mmoja eneo la mkono wa kushoto .
Amesema mara baada ya kumhoji mtoto huyo aliwaeleza kuwa mama
yake mdogo alichukua nguo na mkumfunga mkononi kisha kumwagia maji ya moto
pamoja na kumlazimisha ale kinyesi chake hali ambayo iliwafanya washindwe
kuvumilia na kuanza kupiga kelele kwa lengo la kuomba msaada kwa watu
wengine.
Kwa mujibu maelezo ya mwenyekiti huyo amesema kuwa Mtuhumiwa
huyo amekuwa akifanya vitendo vya manyanyaso kwa mtoto huyo marakwamara ambapo
wamekuwa wakimuonya lakini amekuwa si mtu wa kusikia.
Ameesema mtoto huyo si wa kwa kwakwe kwani amekuwa akiishi naye
kwa muda mrefu sasa ambapo aliachiwa na dada yake ambaye hakufahamika kuwa
nayishi wapi kwa sasa.
Hata Diwani wa kata hiyo Ndugu Samuel Mamboma alifika eneo hilo
tukio na kutoa msaada wa usafiri kwa lengo la kumfikisha mama huyo polisi pamoja
na mtoto huyo ambaye naye alikimbizwa Hospitali.
Hata hivyo amesema tukio hilo si la kwanza kutokea katika meaeno
hayo kwani kumekuwepo na matukio mengi hasa ya utoaji mimba na kutupwa
watoto.
Daaah! Hiyo haiko sawa kabisi inabidi sheria ifuate mkondo kwa huyo mama
ReplyDelete