ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, November 12, 2012

Ujumbe wa wanafunzi wa chuo cha ulinzi cha Taifa Tanzania (National Defence Collage) cha Dar es Salaam Wamtembelea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na ujumbe wa wanafunzi wa chuo cha ulinzi cha Taifa cha Tanzania waliofika ofisini kwake Migombani. Katikati ni kiongozi wa ujumbe huo Brigedia Jenerali JM Mwaseba.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipokea zawadi kutoka kwa kiongozi wa ujumbe wa wananchi wa chuo cha ulinzi cha Taifa huo Brigedia Jenerali JM Mwaseba
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo cha ulinzi cha Taifa Tanzania waliofika ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar.Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
---- 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema suala la amani na usalama ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya nchi na watu wake.
Amesema suala hilo linapaswa kuzingatiwa na kufanyiwa kazi ili kuhakikisha kuwa amani ya Tanzania inaendelea kuwepo wakati wote kwa lengo la kuendeleza sifa ya Tanzania kiusalama, sambamba na kukuza uchumi wa nchi.
Maalim Seif ametoa changamoto hiyo leo ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar alipokuwa na mazungumzo na ujumbe wa wanafunzi wa chuo cha ulinzi cha Taifa Tanzania (National Defence Collage) cha Dar es Salaam, waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha na kubadilishana mawazo.

“kulinda amani ya nchi yetu ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya taifa ya taifa letu, na nachukua nafasi hii kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanzisha chuo hichi”,alieleza.
Amesema nchi zilizoendelea na zina zinazoendelea kwa kasi zilianza kazi ya kulinda usalama wa nchi zao kwa kipindi kirefu, na ndio maana ziliweza kupata mafanikio katika Nyanja mbali mbali za kiuchumi na kijamii.
Amesema ni vyema vyombo vya ulinzi na usalama kuanza kudhibiti viasharia vya uvunjifu wa amani mara vinapogungudua hali hiyo, ili kuiepusha nchi kuingia katika janga la uvunjifu wa amani.
Aidha amesema katika kukabiliana na vitendo vya uvunjifu wa amani serikali inapaswa kujipanga kukabiliana na kero za wananchi hasa ukosefu wa ajira kwa vijana.
Makamu wa Kwanza wa Rais amefahamisha kuwa vijana wengi ambao wamehitimu masomo katika fani mbali mbali bado hawana ajira na kwamba hali hiyo inaweza ikawapelekea vijana hao kufanya vitendo visivyokubalika katika jamii.
Kwa upande wake kiongozi wa ujumbe huo Brigedia Jenerali JM Mwaseba ameelezea matumaini yake kuwa wahitimu wa chuo hicho wataweza kuongeza ujuzi wao katika masuala ya ulinzi na usalama na kusaidia mabambano dhidi ya vitisho na vitendo vya uvunjifu wa amani.
Amefahamisha kuwa wahitimu wa chuo hicho pia watakuwa ni watunga sera wazuri katika taasisi wanazotoka, lengo likiwa ni kuimarisha hali ya usalama na kuimarisha uchumi wa nchi.
Jenerali Mwaseba ameongeza kuwa kozi hiyo ya mwaka mmoja kwa kuanzia imewashirikisha wanafunzi wa Tanzania pekee kutoka taasisi mbali mbali za serikali Muungano na Zanzibar wakiwemo watendaji kutoka Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi na Taasisi za kiraia.

Na 
Hassan Hamad 
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...