Waziri
wa Uchukuzi Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) (pichani) amefuta uteuzi
wa Wajumbe wote wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa
Bandari (TPA) na kuteua Wajumbe wapya wanane wanaounda Bodi hiyo.
Waziri
amechukua uamuzi huo kwa mujibu wa Sheria ya Bandari na Kifungu cha
1(2)(i) cha Jwdwali la Kwanza la Sheria ya Bandari ya 2004.
Mabadiliko
hayo ni sehemu tu ya hatua ambazo Wizara inachukua kurejesha ufanisi
katika Mamlaka hiyo ili iweze kuchangia zaidi kwenye pato la Taifa.
Aidha
Waziri ameiagiza Menejimenti ya TPA kuwapa nyaraka zote muhimu Wajumbe
wa Bodi ili wajiandae kabla hajakutana nao ndani ya simu 10 ili kuingia
nao Mkataba wa Ufanisi (Performance Contract).
Waliofutiwa Ujumbe wa Bodi ni:
1. Bw. Dunstan G. Mrutu.
2. Eng. George H. Ally.
3. Mh. Alh. Mtutura A. Mtutura (Mb).
4. Bw. Emmanuel Mallya.
5. Bibi Mwanmtumu J. Malale.
6. Bibi Maria N. Kejo.
Kwa bahati mbaya wajumbe wawili wa Bodi hii walipoteza uhai hivi karibuni.
Walioteuliwa kuingia kwenye Bodi hiyo ni:
1. Dkt. Jabiri Kuwe Bakari.
2.Bw. John Ulanga.
3. Bi. Caroline Temu.
4. Bw. Jaffer Machano.
5. Dkt. Hildebrand Shayo.
6. Bw. Saidi Salum Sauko.
7. Eng. Julius Mamiro.
8. Bi. Asha Nassoro.
No comments:
Post a Comment