Huyu ndiye Bilawal Bhutto mtoto wa marehemu
Benazir Bhutto aliyeuwawa na Talebana 2007 na pia ni mtoto wa rais
Asif Ali Zardari ambaye ni rais wa sasa wa Pakistan. Bilawal anaandaliwa kushika wadhwa urais wa Pakistan
Benazir Bhutto aliyeuwawa na Talebana 2007 na pia ni mtoto wa rais
Asif Ali Zardari ambaye ni rais wa sasa wa Pakistan. Bilawal anaandaliwa kushika wadhwa urais wa Pakistan
Akiwa kwenye shughuli za kisiasa
Akiwa chuo kikuu cha Oxford
Rais Asif Ali Zardari akinyanyua mkono wa mwanae Bilawal Bhutto kumtambulisha
Aliwa kwenye mavazi ya kijadi
Akiomba dua
Mwanawe waziri mkuu wa Pakistan aliyeuawa, Benazir
Bhutto, anazindua kuingia kwake kwenye siasa hii leo ikiwa ni
maadhimisho ya mwaka wa tano tangu mamake kuuawa.
Bilawal Bhutto Zardari anatarajiwa kutangaza
malengo yake kwa mara ya kwanza mbele ya maelfu ya wafuasi nyumbani mwao
katika jimbo la Sindh. Mamia ya maelfu ya wafuasi wa chama cha Pakistan Peoples Party walianza kufurika Larkana kabla ya siku hiyo kubwa.
Wanaharakati waliobeba picha za Benazir Bhutto, na babake, waziri Mkuu wa zamani Zulfiqar Ali Bhutto, wamekita kambi kote mjini humo.
Chama hicho tawala kinataka kutumia sherehe hiyo kuonyesha kuwa licha ya shutuma kuhusu utendakazi wake katika miaka mitano iliyopita, bado kina wafuasi wengi.
Hotuba kuu itatolewa namwanawe Bhutto, Bilawal Bhutto Zardari.
Itakuwa mara ya kwanza kwake kuhutubia mkutano wa maelfu ya wafuasi kuelezea maono ya chama hicho.
Aliteuliwa mwenyekiti wa chama hicho punde tuu baada ya kuuwawa kwa mamake na wapiganaji wa taliban mwaka wa 2007, lakini hajajitokeza hadharani kutokana na umri wake mdogo na kukosa uzoefu wa kisiasa.
Huku uchaguzi wa Bunge ukitarajiwa Pakistan katikati ya mwaka wa 2013, waliochoshwa na siasa za rais Zardari, wanamuangalia, kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 na aliyehitimu kutoka chuo cha Oxford, kufufua umaarufu wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment