Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia gari ya
Paroko wa Parokia ya Mpendae Padre Ambrose Mkenda ambayo alikuwa
akiendesha na kuvamiwa kwa risasi ya watu wasiojuilikana
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar akipata maelezo kutoka kwa Uongozi wa Skuli
ya Francis Maria Tomondo ambapo Padre Ambrose Mkenda wa Paroko ya
Parokia ya Mpendae alijeruhiwa kwa risasi hivi karibuni
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifuatana na Askofu
Shao wa Kanisa la Roman Catholic liliopo minara miwili baada
kuwafariji na kutoa mkono wa pole kwa uongozi wa huo kufuatia
kujeruhiwa kwa Paroko wa Parokia ya Mpendae Padre Ambrose Mkenda.
---
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi alifika katika makazi ya padri Ambrose Mkenda wa
Paroko wa parokia ya kanisa katoliki la Mpendae Zanzibar kuupa pole
uongozi wa Kanisa hilo pamoja na Familia yake kufuatia ajali ya kupigwa
risasi hivi karibuni na watu wasioujulikana.
Tukio hilo la kusikitisha lililofanywa
na watu wawili waliopakiana kwenye Vespa lilitokea langoni mwa Skuli ya
Francis Maria iliyopo Tomondo Wilaya ya Magharibi ambapo ndio makaazi
ya Padri Ambrose.
Balozi Seif akiufariji Uongozi huo alisema ni jambo baya na la
kusikitisha lililofanywa na watu hao ambalo limetoa sura mbaya kwa
Taifa na Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi itaendelea kufanya
uchunguzi wa tukio hilo na haitasita kuwachukuliwa hatua za kisheria
watu watakaobainika kufanya uhalifu huo.
Alisema Serikali imesikitishwa na kulaani kitendo cha watu hao ambacho
kinaashiria uvunjifu wa amani pamoja na kuwaweka wananachi katika hali
ya wasi wasi usio wa lazima ndani ya harakati zao za kimaisha.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Uongozi na Familia ya Padre Ambrose Mkenda
Kiongozi kutoka Kanisa la Roman Catholic Askofu Shao aliiomba Serikali
kuendelea kuimarisha ulinzi wa raia wema ili kupunguza hofu iliyotanda
mioyoni mwao kutokana na matukio ya uvamizi
Askofu Shao alitahadharisha kwamba hulka mbaya iliyoanzishwa na baadhi
ya watu kuwafundisha watoto wadogo tabia ya kukashifu watu wazima kwa
sababu ya utofauti wa Kidini inawajengea maisha mabovu watoto hao.
“ Watoto wadogo kufundishwa tabia ya kukashifu watu wengine tuelewe
kwamba Taifa halitakuwa na muelekeo mwema wa jamii yake ya baadaye”.
Alitahadharisha Askofu Shao.
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
No comments:
Post a Comment