CHADEMA Mkoa wa Arusha yapata vyombo vya Muziki kwa ajili ya Mikutano.
Aliyekuwa
mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa anawashukuru
wanachini na wadau ambao walifanikisha ununuzi wa vyombo vya chama mkoa
wa Arusha wakati walipokuwa wameudhuria kwenye event ya M4C-JOIN
THECHAIN iliyofanyika katika ukumbi wa hotel ya Snowcrest jijini Arusha.
Lema
akiwa na baadhi ya wanachama ambao ni wadau wakubwa wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema ambapo alisema kuwa wadau hawa
wanatarajia kuingia katika majimbo mbalimbali hapa nchini kwa ajili ya
kuwaletea watanzania ukombozi
Hawa ndio wanakamati waliofanikisha ununuzi wa vyombo vya M4C JOIN THE CHAIN.
Viongozi wa vyama mbalimbali wa mkoa wa Arusha chadema waliohudhuria sherehe hiyo.
Wadau
mbalimbali waliohudhuria katika shughuli ya uchangiaji wa vyombo vya
muziki ambapo vilipatikana na uchangiaji wa gari la kubebea vyombo
hivyo ambapo wageni waliohudhuria katika shughuli hiyo waliahidi
kutoa shilingi milioni 27 kwa ajili ya ununuzi wa gari la kubebea vyombo
mdau kama ukiguswa unaruhusiwa kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa
gari hilo ambalo ni kwa ajili ya kuendesha gurudumu M4C JOIN THE CHAIN
unachotakiwa kufanya ni kufika katika ofisi za chama cha Demokrasia na
maendeleo zilizopo mkoani Arusha na utoe mchango wako.
katika shughuli hiyo vinywaji vilikuwa vya kumwaga.
Mwanadada
Aminata Saguti yeye alitoa mada ila kilio chake kikubwa kilikuwa ni kw
awanawake aliwasihi wanawake watoe dhana ya woga na waanze kazi
wajiamini nawasiogope kugombea nafasi mbalimbali uongozi katika vyama na
hata nchi pia alisema kuwa yeye binafsi anajiamini na anampango wa
kugombea jimbo moja lililopo mkoani Tanga ifikapo mwaka 2015 kwani jimbo
hilo limekuwa likiendeshwa kwa muda mrefu na watu ambao hawajawasaidia
wananchi kitu chochote na wananchi wa jimbo hilo wanazidi kuteseka kila
siku japo kuwa wanambunge wao.
Mbunge
wa jimbo la Arumeru Magharibi Joshua Nasaari akibadilishana mawazo na
aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini wakati shughuli ikiendelea
ambapo mbunge nassari yeye alitoa shilingi milioni mbili kwa ajili ya
ununuzi wa gari la kubebea vyombo vya muziki.
Kulikuwa pia na nyimbo za
chama cha demokarasia na maendeleo zinapigwa hivyo kila mmoja alionyesha
furaha yake ya kucheza na kufurahia chama chake.
Pia katika shuhuli hii
kulikuwa na watoa mada mbalimbali kuhusianana mapinduzi mwanadada
Kaithari Mohamed ni mpiganaji wa chama cha demokrasia namaendeleo
Chadema yeye aliwahamasisha wanawake kujitambua nakujua haki zao na nini
maana ya mapinduzi alisema kuwa mwanamke asifiwi kwa uzuri wa nje
,gari alilonalo ,nyumba aliyonayo wala umaarufu alio nao bali ni nini
alichoifanyia jamii iliyo mzunguka hivyo aliwasihi wamama wajitokeze kwa
wingi kupigania haki zawatanzania na wajitambua huku akikumbushia kuwa
ata Nelson Mandella alisaidiwa na mke wake ndo maana akashinda na uhuru
ukapatikana hivyo wanawake wanaweza na sio mpaka wawezeshwe bali
wanaweza wenyewe.
Kwa
upande wake Katibu wa mkoa Chadema Amani Golugwa (Pichani) aliwashukuru
sana wadau wote ambao wamehudhuria na kushiriki katika shughuli hii ya
kuchangia vyombo pamoja na kuchangia gari la kubebea vyombo na
alibainisha kuwa wakati huu ni wa mabadiliko wanafanya kazi kw akusonga
mbele na hawatakubali kurudishwa nyumba huku akibainisha kuwa wakati huu
sio wakuulizana nani mwizi bali ni wakati wa kukamata mwizi nakufanya
kazi tu.
Alisema
kuwa swala la mabadililiko ni mpango wa Mungu hivyo hakuna mtu yeyote
ambaye anaweza kuzuia mipango wa Mungu akisema kuwa wanajua itachukuwa
muda lakini lazima mabadiliko yatatokea tu.
Aliongeza
kuwa kwakipindi hichi wameamua kuanzisha M4C JOIN THE CHAIN hiii ikiwa
ni njia ya kuleta mabaidiliko huku akisema kuwa wanataka wanyakuwe
majimbo yote ya mkoa wa Arusha.
“unajua
tunataka tunyakuwe majimbo yote ya mkoa wa Arusha nakwanza kabla ya
kuyachukuwa tunataka tuanze kuwaonyesha wananchi katika baadhi ya
halmashauri tulizo zichukuwa ambapo alisema kuwa wao kama chadema mkoa
wa Arusha wanamiliki halmashauri mbili ambayo ni halmashauri ya Meru
pamoja na Karatu ambapo alisema hizi ndio anataka ziwe za mfano katika
kuleta maendeleo.
Alifafanua kuwa vyombo vya mziki vilivyonunuliwa (Pa
system)viligharimu kiasi chashilingi milioni 14 na laki sita ,huku
kiasi cha shilingi milini 27 zikiwa ni ahadi kwaajili ya gari na keshi
ikiwa ni shilingi milioni moja
No comments:
Post a Comment