Mkurugenzi Mtedaji wa Vodacom Rene Meza akihutubia
katika mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF) mjini
Tanga mwishoni mwa wiki. Rene alitumia nafasi hiyo kuzungumzia uwekezaji
wa Vodacom hapa nchini na mchango wa kampuni hiyo katika uchumi wa nchi
na maendeleo ya ustawi wa Jamii.
Christina Chambo wa
Kituo cha Comfort akiongoza sala ya ufunguzi wa hafla ya utoaji zawadi
ya Krismasi kwa watoto wa kituo hicho cah Comfort na Diana vyote vya
Mjini Tanga vilivyotolewa na wafanyakazi wa Vodacom kupitia kampeni
ya Pamoja na Vodacom. Zaidi ya Sh. 50 Milioni zitatumika katika kampeni
hiyo na kunufaisha makundi yenye uhitaji sehemu mbalimbali nchini.Meza
Kuu kutoka kushoto ni Bi Martha, Yessaya,Rene, Saanani na aliyesimama
kulia ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzaniia (TEF) Tefil Makunga
akimtambulisha Mkurugenzi Mtedaji wa Vodacom Rene Meza (wa pili kushoto)
kabla ya Rene kuhutubia mkutano mkuu wa mwaka wa TEF mjini Tanga mwishoni
mwa wiki. Rene alitumia nafasi hiyo kuzungumzia uwekezaji wa Vodacom
hapa nchini na mchango wa kampuni hiyo katika uchuni wa nchi na maendeleo
ya ustawi wa Jamii. Kushoto ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum
Mwalim
Mkurugenzi Mtendaji
wa Vodacom Tanzania Rene Meza akikabidhi zawadi ya krismasi kwa watoto
wa kituo cha malezi kwa watoto wenye mahitaji cha Comfort kilichopo
eneo la Majani Mapana Mkoani Tanga zilizotolewa kupitia program ya Pamoja
na Vodacom (zamani Care & Share) inayoendeshwa na Vodacom Foundation
nyakati za sikuu kuu ya Krismasi. Kulia ni Mwakilishi wa Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Masoud Saanani na Meneja wa Vodacom Tanga Mjini
Edgar Malimbo. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na waharii mbalimbali ambao
walikuwepo mkoani Tanga katika kkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri
Rene (mwenye koti jeusi
katikati) pamoja na watoto wa kituo cha Comfort wakiwa katika picha
ya pamoja na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari walioshiriki
katika hafla ya ukabidhi zawadi ya Krismasi kwa vituo vya Comfort na
Diana vya Mkoani Tanga. Wafanyakazi wa Vodacom wamekusanya kiasi cha
Sh. 50 Milioni kusaidia watoto yatima na Makundi mengine yenye uhitaji
kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom.
No comments:
Post a Comment