ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Tuesday, December 4, 2012

Eneagram: Perfectionsit / Hasira


Enneagram ni chombo cha saikolojia  kinachotumika kujifunza  juu ya tabia za Binadamu. Ni elimu inayotusaidia sisi kujifahamu kwa ndani. Kutambua tabia zetu za pekee na kukua katika njia ya kujipenda na kuwapenda wengine. Kwa kawaida tunawapima wenzetu kama tunavyowaona. Tunawakosea wenzetu kwa sababu hatufahamu jinsi waavyojifahamu. Hivyo Eneagram itatupa uwezo wa kutusaidia kukua katika mambo ya kimahusiano na hata katika mambo ya kiroho.
Hapo ulipo kama nilivyosema awali, hauwezi kukwepa kukaa katika makundi ya watu uwapo kazini, shuleni, mazoezini, makambini n.k. Ukae ukijua kwamba, hakuna watu wawili walio sawa. Hata mapacha ambao wanafanana sana hawako sawa. KILA MMOJA NI WA PEKEE. Kwa maana hiyo, kila mmoja katika watu unaoishi nao ana tabia yake ya pekee na njia yake ya pekee ya kufanya kila kitu. Kila mtu anatazama maisha yake kwa njia maalum. Katika maisha, kila mtu anachagua matendo kwa kufuata mwelekeo wake, tabia yake.
Katika mduara wa Eneagram, kuna aina tisa za tabia zinazoeleza njia mbalimbali 9 ya matendo yetu. Kila mtu anayo namba yake, au sehemu yake, ingawa tangu utoto wetu tumekuwa tukiitikia mwito wa maisha kwa njia moja tu. Tulianza kufuata njia hii tukiwa wagogo, na ilitusaidia kufaulu katika maisha yetu na tukaendelea kuitumia. Kwa kuwa tuliitumia mara kwa mara, tukaizoez na ndiyo ikawa tabia yetu hata tulipokuwa watu wazima na zaidi hata tulipokuwa kati ya watu. "ni tabia yangu sasa nifanyeje" "Ndivyo nilivyo so what" "ndivyo nilivyoumbwa"
Eneagram ni kama Kichujio, au tinted class zinazosaidia kupunguza ukali wa jua. Enegram inatupa mazoezi ya kubadili yale yanayowezekana kwa sababu tunafikia mahali ambapo sasa tabia yetu inakuwa ni kama MSHURUTISHO / COMPULSION (TUNAFANYA HATA BILAKUFAHAMU)


Kama nilivyoahidi, leo nitazungumzia tabia ya kwanza.
1. PERFECTIONIST; (tatizo lake kubwa ni hasira)
Haki yangu ya ndani ni ya usahihi kabisa. Inabidi kuishi katika hali ya usahihi tu. Ni rahisi kwangu kuona mapungufu  na makosa wa watu wengine au katika vitu mbalimbali wanavyofanya wengine. Mimi naona kama ninaweza kuvifanya vikawa vizuri zaidi hata kama hivyo vilivyofanywa ni vizuri kiasi gani. Watu wengine wananichukulia kama mjuaji, au kama mtu anayetaka kila kitu kiwe zahihi tu bila kosa lolote. Bila waa lolote. Kama kitambaa cheupe kisichouwa na doa. Ninajisifu kwamba nikifanya jambo fulani, au nikipewa jukumu lolote basi nina uhakika nitafanya yote kwa ukamilifu mkubwa. Ninasikia hasira na kuwalaumu wengine wasipofanya mambo kwa ukamilifu kama mimi, au wasipowajibika ipaswavyo. Mathalani, mimi mimeingia ofisini asubuhi, nikaandaa kazi zangu nikazifanya haraka na kwa usahihi mkubwa sana. Wakati huo huo wenzangu wanapiga story au wako busy na blackbery zao, basi nasikia hasira sana. Mwanzoni najitahidi kutokuonyesha hadharani ingawa naumia sana. Kwa kawaida kwangu kazi ni muhimu kwanza kabla ya kitu chochote halafu baadaye ndo nipumzike au nifanye vitu vya anasa. Najinyima hata chakula cha mchana ilimradi tu kazi niliyopewa na bosi ifanyike tena kwa ufasaha kabisa.
Baada ya maelezo hayo utaweza kuona kwamba, mtu mwenye tabia hii kama yuko ofisini kwako atapendwa sana na bosi wake wa kazi, na uwepo wake ni kikwazo kwa wengine kwani pamoja na kwamba anafanya apaswayo kufanya lakini atatumika sana na wengine wanaweza kuumizwa kwa sababu yake.
Kosa lake kubwa ni nini? MSHURUTISHO/COMPULSION yake ni;
KUJISIKIA RAHA AU MVUTO KUSAHIHISHA MAKOSA YA WENGINE NA YEYE NI MTU ASIYEKUWA NA MAKOSA KAMWE, HIVYO HATA KAMA AMEKOSEA KIUKWELI HATOKUBALI KUSAHIHISHWA KWANI YEYE ANAAMINI HAFANYAGI MAKOSA.
Mwishobaada ya kueleza tabia hadi ya tisa, nitaeleza ni mtu wa tabia ipi ataweza kuishi vizuri na perfectionist. Na pia perfectionist anaweza kujirekebishaje?

Kesho tutaongelea namba 2: Giver/Mtoaji (tatizo kale kubwa ni Kiburi)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...