
Waziri
wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza
Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara ya Madini (TAMIDA), Bw. S. Sammy
Mollel walipokutana katika makao makuu ya Wizara ya Nishati na Madini
ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na biashara ya madini
nchini ikiwa ni pamoja na ufungaji na usafirishaji wa vifurushi na
mizigo ya madini, ongezeko la kodi ya thamani ya asilimia 18 ya madini,
bei elekezi ya uuzaji wa madini inayotolewa na TANSORT, ada za leseni za
wafanyabiashara na uombaji wa kibali maalumu kwa watalii wanaonunua
madini ya vito kwenye maduka ya vito.

Waziri
wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akitoa ufafanuzi wa
baadhi ya hoja zilizokuwa zikijadiliwa na Wafanyabiashara wa Madini
nchini ambapo aliunda kamati maalumu ambayo itahusika na upangaji wa bei
elekezi ya madini. Kamati hiyo itahusisha wajumbe mbalimbali kutoka
wizarani, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wawakilishi kutoka Chama
cha Wafanyabishara ya Madini nchini (TAMIDA). Kamati hiyo itaongozwa na
Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthamini wa Almasi na Vito Tanzania. (TANSORT)
No comments:
Post a Comment