
Hugo Chavez akiwa hana nywele baada ya kutumia dawa za chemotherapy kwa ajili ya kutibu kanser

Chavez akiongea na waandishi wa habari akiwa na Nicolas Maduro pembeni


Chavez akiwa na Castro

Nicolas Maduro mrithi wa Hogo Chavez


Maduro aliyekuwa dereva wa basi sasa anatarajiwa kuwa rais wa Venezuela ikiwa Hogo Chaves atashindwa kutokana na ugonjwa wa Kansa unaomsumbua
Rais wa Venezuela Hogo Chaves amewaambia wananchi wa Venezuela jana kuwa, ugonjwa uliokuwa unamsumbua wa kansa umerejea tena. Chaves ambaye alienda Cuma kwa siku kumi kwa ajili ya kuchunguza tena afya yake amerudi jijini Caracas na kuweka wazi zaidi kwa mara ya kwanza kuhusu kansa ambayo awali ilikuwa imedhibitiwa na madaktari wa Cuba.
Caves mwenye umri wa miaka 58 sasa amekuwa kiongozi mwenye msimamo mkali kuhusu sera za mafuta na sera za mambo ya nje, amekuwa akipingana waziwazi na maamuzi yanayofanywa na mataifa ya Magharibi na Marekani.
Chavez ambaye amechaguliwa tena kuiongoza Venezuela kwa kipindi kingine cha miaka 6 anatarajiwa kuapishwa rasmi tarehe 10 januari lakini duru za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa huenda kuapishwa kwake kukaahirishwa kutokana na ugnjwa wake na kwa kuwa atakuwa anafanyiwa matibabu huko Cuba.
Kwa mara ya kwanza Chaves ameweka wazi kwamba, kama hali yake ya afya itaendelea kuwa mbaya kiasi cha kushindwa kuiongoza Venezuela basi achaguliwe makamu wake wa rais Bwana Nicolas Maduro. Maduro ambaye awali alikuwa dereva wa mabasi, alikuwa msemaji mahiri sana wa Chaves kabla ya kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje kwa kipindi kirefu na hivi karibuni akateuliwa kuwa makamu wa rais.
No comments:
Post a Comment