ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, December 10, 2012

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Sekretarieti Wakutana na Makatibu wa CCM wa Mikoa Leo Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao chake cha Sekretarieti na Makatibu wa CCM wa mikoa, leo, Desemba 11, 2012, katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na wengine kutoka kushoto ni Makatibu wa NEC,  Asha-Rose Migoro (Siasa na Mambo ya Nje), Zakia Meghji (Uchumi na Fedha), Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao chake cha Sekretarieti na Makatibu wa CCM wa mikoa, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai akisalimiana na Katibu wa NEC, Siasa na Mambo ya Nje, Asha-Rose Migiro, kabla ya kuanza kikao cha Sekretarieti na Makatibu wa CCM wa mikoa, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Muhammed Seif Khatib.
Makatibu wa CCM wa mikoa wakiwa kwenye mkutano wao na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.Picha na Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...