Mbunge wa Arusha Mjini-CHADEMA,Godbless Lema akisalimia wananchi wa Arusha jana
..akiwapa saluti wapiga kura wake kwa uvumilivu
..........wapenda sana wanaarusha.
---
Na Mroki Mroki-Arusha
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema amewaahidi wapiga kura
wake kutoendelea na siasa za maandamano na badala yake sasa ni kazi tu na
mijada la malalamiko yote ni katika vikao.
Akihutubia wananchi, alisema yuko tayari kuwatumikia Wana-Arusha huku
akiahidi kuwa hatoandamana tena, bali madai na kero zake atazielekeza kwenye
vikao ndani ya Halmashauri.
Alisema akiwa madarakani, hatapenda kuona watu wakiteswa na wanamgambo wa Jiji,
hasa wanawake na wafanyabiashara ndogoo na kusisitiza kuwa, hayasemi hayo kwa
lengo la uchochezi, bali kama angalizo kwa kuwa siku zote yupo kwa ajili ya
kupigania haki na hatarudi nyuma kwa hila yoyote.
Kabla ya kukaribishwa kuzungumza na wananchi, Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, alisema chama chake kimefanya tathimini ya kesi iliyomalizika na kusema wanatarajia kudai fidia ya gharama za kesi hiyo inayofikia Sh milioni 253.
Golugwa pia alitumia muda huo kumkabidhi bendera ya Bunge Lema ambayo alikabidhiwa na Mbunge huyo baada ya kuvuliwa nafasi hiyo Aprili mwaka huu.
Alisema alipokabidhiwa bendera hiyo alimwambia aiweke na kusubiri Mungu atende muujiza ambao kwa sasa anasema umetimia kwa Lema kurudishiwa ubunge.
Kuhusu madiwani waliofukuzwa Chadema, alisema kuwa bado anaamini walitendewa haki ya kufukuzwa sababu ya kurubuniwa na huku akiahidi kuwa, uchaguzi ukirudiwa chama chake kitaibuka na ushindi mnono.

No comments:
Post a Comment