ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Sunday, December 23, 2012

Mkutano Kati ya Ujumbe kutoka Tanzanaia na Watanzania waishio Oman (Diaspora)Wafana Jijini Muscat.

 
Picha ya Meza Kuu katika ufunguzi wa Mkutano wa Diaspora. Kutoka kushoto walioketi ni Bw. Michael Kmba (AG Chambers), Balozi Bertha Semu-Somi, Balozi Ali Saleh (Balozi wa Tanzania-Oman), Balozi Yahya Simba(Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati), Bw. Olal Kungu (Kamishna-Hazina)na Bw. Shariff Sharrif(Mkurugenzi-ZIPA
Bw. Hassan Hafidh (katikati) kutoka Ofisi ya Rais-Diaspora Zanzibar, akizungumza na wadau wa Diapsora juu ya mipango ya Serikali ya Mapinduzi wa Zanzibar kwa Watanzania wenye asili ya Zanzibar waishio nje.
Bw. Boniface Ngowi wa Wizara ya Viwanda na Biashara akitoa maelezo kwa Watanzania waishio Oman kuhusu Sera za Biashara nchini Tanzania.
Bi. Patricia Nguma (kulia), kutoka Benki ya Afrika (BOA), akijadiliana na Mdau wa Diaspora kuhusu mikopo ya nyumba inayotolewa na BOA.
Balozi Simba Yahya (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akipokea maoni kutoka kwa Watanzania wenye asili ya Oman kuhusu ushiriki wao kwenye maendeleo ya kuinua uchumi nchini Tanzania.
Baadhi ya Watanzania waishio nchini Oman wakisikiliza kwa makini wakati wa Ufunguzi wa Mkutano unaoghusia masuala ya Diaspora yakiwemo uwekezaji katika sekta mbalimbali za kuinua maendeleo ya uchumi nchini Tanzania.Picha na Habari Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
--
Mkutano kati ya Ujumbe wa Tanzania na Watanzania waishio Oman ulioanza tarehe 20 umemalizika leo jijini Muscat, Oman. Ujumbe wa Tanzania unaoongozwa na Balozi Bertha Semu-Somi, Mkurugenzi wa Masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na unajumuisha wajumbe kutoka Wizara za Mambo ya Nje, Fedha, Viwanda na Biashara, Nishati na Madini, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Miundombinu, Habari na Utamaduni, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,Afisi ya Rais inayoshughulikia masuala ya Diaspora Zanzibar na Tume ya Mipango Zanzibar. Aidha, ujumbe umehusisha Taasisi za Serikali za TBC,TIC,TCRA, EPZA, ZIPA, UHAMIAJI, TTB,TANAPA na Dar es Salaam Maritime Institute. Ujumbe huu umejumuisha pia wajumbe kutoka Sekta Binafsi zikiwemo TPSF, BOA, Azania Bank, CRDB, PBZ, Uhuru One, Zanzibar Issurance Corporation na Zanzibar Chamber of Commerce.

Mkutano wa Diaspora umeitishwa kufuatia maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano uliopita kati ya Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Watanzania waishio Oman ambapo aliwashawishi kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa Tanzania. Mhe. Rais aliwaahidi kutuma timu ya wataalamu kukutana na Diaspora kuwajulisha juu ya fursa zilizoko nchini na kupokea changamoto zao zinazowakwamisha kuchangia katika uchumi wa Tanzania.


Katika kikao hicho kilichomalizika leo, watanzania waishio Oman wamepata fursa ya kukutanishwa na taasisi za Tanzania na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ikiwemo kuanzisha mawasiliano yenye lengo la kukuza ushirikiano wa kibiashara. Masuala yaliyojitokeza ni pamoja na haja ya kuanzishwa kwa Chama cha Watanzania waishio Oman.


Oman ni nchi ambayo wananchi wake wengi wana asili ya Tanzania kutokana na uhusiano wa kihistoria baina ya nchi hizi mbili. Inakadiriwa kuwa familia 780 za Watanzania wanaishi nchini Oman na kuendesha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...