Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Monduli juu,Mkoani Arusha wakati
alipokuwa akiwasili kijijini hapo kwa ajili ya shughuli ya uzinduzi wa
josho la kisasa la Mifugo katika kijiji cha Mfereji Monduli juu.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akikaribishwa kwenye kijiji cha Mfereji Monduli juu,wakati alipokuwa
akiwasili kijijini hapo kwa ajili ya shughuli ya uzinduzi wa josho la
kisasa la Mifugo.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akifunua
kitambaa kwenye jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa josho la kisasa la
Mifugo,lililoko katika Kijiji cha Mfereji,Monduli Juu.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mfereji,Monduli Juu,mara baada ya
kuzindua josho la kisasa la Mifugo.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo,lililoko katika
Kijiji cha Mfereji,Monduli Juu.
Mifugo ikiingizwa kwenye Josho hilo,mara baada ya kuzinduliwa.
Wakazi wa kijiji cha Mfereji,Monduli juu wakimsikiliza Mh. Lowassa (hayupo pichani).
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Monduli juu,Mkoani Arusha wakati
wa hafla ya uzinduzi wa josho la kisasa katika kijiji cha Mfereji
Monduli juu. ambapo ametoa wito kwa wakulima na wafugaji nchini kuacha
uhasama wa kugombea ardhi.
Amesema kuwa kila mtu ana
haki yake hivyo ni muhimu kwa jamii hizo kuheshimiana na kukaa pamoja
kutatua tatizo la ardhi kwa ajili ya malisho ya mifugo pamoja na
kilimo.Kumekuwa na matokeo mengi sehemu mbalimbali ya kupigana kuwania
ardhi kati ya wakulima na wafugaji, miongoni mwa maeneo hayo ikiwa ni
mkoani arusha.
Amewaambia watu wa jamii ya kimasai ambao ni wafugaji kuingia katika ufugaji wa kisasa utakaowazuia kuhama hama kutafuta malisho ya mifugo yao.”Jamani watanzania wenzetu hawatakubali mtakapovamia maeneo yao bila ya ruhusa ni lazima tuondokane na tabia hii” alisema.

No comments:
Post a Comment