Afisa
habari Ngazi ya Taifa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC)
Bi. Usia Nkhoma akitoa maelezo ya awali kuhusiana na mafunzo hayo
yanayolenga kuwawezesha vijana kuwa na uelewa na mbinu juu ya
ujasiriamali na namna ya kusimamia biashara zao ili kuongeza uzalishaji
hivyo kupambana na kuupunguza umasikini katika ngazi zao kabla ya
kumkaribisha Mratibu wa Taifa wa Mradi wa ILO wa Ujasiriamali kwa vijana
Bw. Louis Mkuku (kushoto).Ameongeza kuwa pamoja na kupata uelewa juu ya
ujasiriamali mafunzo hayo yanakwenda sambamba na lengo namba 1 la
Maendeleo ya Milenia ambalo ni Kupunguza Umasikini, kwa kuwa yatawapatia
mbinu zitakazowawezesha kuboresha shughuli zao za kujipatia kipato
hivyo kuwa na kipato endelevu.
Mratibu wa Taifa wa Mradi wa ILO wa Ujasiriamali kwa vijana Bw. Louis
Mkuku akifungua rasmi mafunzo hayo ambapo ametoa hamasa kwa vijana
kutumia vizuri elimu watakayoipata wakati huu wa ujana wao kujenga
maisha ya baadae na kuahidi kufuatilia kwa umakini matokeo ya mafunzo
hayo na kusema atahakikisha kila mwenye ndoto itatimia kwa usimamizi wa
ILO na UNIC.
Pichani
Juu na Chini Washiriki wa Mafunzo ya Siku moja ya Ujasiriamali
wakisiliza nasaha za mgeni rasmi wakati akifungua rasmi mafunzo hayo.
Bi. Mary France kutoka Best Alternative Consulting and Marketing
Company (BEACOM) akizungumzia mada ya Ujasiriamali katika usimamizi wa
biashara ambayo ndio sehemu nyingi wafanyabiashara wadogo ndipo
wanapokwama kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha.
Pichani
Juu na chini ni Bi. Tusnime Kyando kutoka BEACOM akifundisha kwa
nadhiria kuhusu swala la uchambuzi wa biashara na gharama za biashara
ambayo mjasiriamali anakusudia kuifanya ili aweze kujua ataanzia wapi na
aelekee wapi.
Mshauri
kutoka BEACOM Bw. Masudi Kandoro akiwaelezea washiriki wa mafunzo hayo
ni namna gani wanaweza kupanga matumizi ya fedha waliyonayo ili iweze
kukidhi mahitaji ya wanachotaka kufanya.
Bi. Usia Nkhoma akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Wanawake
Tanzania Bi. Magreth Chacha (katikati) kuzungumza na vijana
wajasiriamali. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Access Insurance Agency
Tanzania Ltd. Bw. Gadi Kalugendo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania Bi. Magreth Chacha akielezea jinsi
wajasiriamali wadogo wanavyoweza kupata mikopo katika benki yake, aina
za mikopo inayotolewa, vigezo vinavyoangaliwa, taratibu zinazofuatwa na
taratibu za marejesho ambapo pia amesema japo benki hiyo inatoa
kipaumbele kwa wanawake lakini pia wajasiriamali wanaume wanaweza
kujiandikisha na kupata mikopo.
Pichani
Juu na Chini baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali wakishiriki
kutoa maoni na kuuliza maswali wakati mafunzo hayo yakiendelea.
Ukumbi
wa Mikutano wa Shirika la Kazi Duniani ukiwa umefurika vijana kutoka
vikundi mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakipata elimu ya mafunzo ya
Ujasiriamali yaliyoendeshwa na Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
No comments:
Post a Comment