
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia Rais Mwai Kibaki wa
Kenya akimkabidhi nyundo Rais Yoweri Muzeveni kama ishara ya kukabidhi
Uienyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kijana Joel
Adagson Mwigomole kwa kuibuka mshindi wa pili wa kuandika Insha kwa
wanafunzi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa
mkutano wa nne wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya. Joel ni mwanafunzi wa kidato cha
tatu katika shule ya sekondari ya Mzumbe, Morogoro.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Yoweri
Museveni wa Uganda akimpongeza kijana Joel Adagson Mwigomole kwa kuibuka
mshindi wa pili wa kuandika Insha kwa wanafunzi wa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa nne wa Jumuiya
hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini
Nairobi, Kenya.Joel ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya
sekondari ya Mzumbe, Morogoro.


Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa nne wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini
Nairobi, Kenya


Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na
viongozi wenzie wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na washiriki mwishoni
mwa kikao cha nne cha Jumuiya nje ya Jengo la Mikutano wa Kimataifa la
Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa kwa heshima wakati anaondoka jijini Nairobi, Kenya.Picha na IKULU
No comments:
Post a Comment