
Raia mmoja wa
Ubelgiji aliyetambulika kwa jina moja tu Jan, amekuwa akifanyiwa matibabu ya
akili baada ya kuathirika kisaikolojia
baada ya kugundua kuwa mwanamke aliyefunga naye ndoa miaka 19 iliyopita alikuwa
ni mwanaume aliyejibadilisha jinsia. Jan mwenye umri wa miaka 64 kwa sasa
amekuwa akilalamika kutaka kuachana na mwanamama hiyo. Hata hivyo jaribio la
kisheria la kutaka kuachana na janajike hiyo lakini amegonga mwamba kwa kuwa
mahakama moja ya Ubelgiji imekataa hadi sasa kutengua ndoa hiyo kwa kuwa mama
huyo (Monica) anatambulika kisheria kama mke wa ndoa. Bwana Jan amejitetea
kwamba Monica raia wa Indonesia walikutana mwaka 1993 na kujiridhisha kuwa ni
mwanamke mrembo na bora wa kuwatunza watoto wake na hata kuzaa naye watoto.
Jana anadai kuwa Monica alitumia nyaraka za uongo na majina feki ili
kukamilisha azma yake ya kuolewa na aweze kuishi kama mwanamke. Jan alimuoa
Mocica baada ya mkewe wa awali kufariki na kumwachia watoto wawili ambao
walikuwa wakiishi naye kwa ukiwa na ndipo alipoamua kumwoa Monica, alisema
mwanasheria wa Jan Verjau Liliane.
Jan, alisema
kuwa yeye na mke wake Monica walliamua
kuoana na wakakubaliana kutokuwa na watoto kwani yeye tayari alikuwa na watoto
wawili na mke wake ambaye alishafariki. Jan aliendelea kusema kwamba Monica
alikuwa akimdanganya na wakati mwingine alikuwa akitumia pedi kujikinga na damu
ya hedhi ili kuficha ukweli. "Hata wakati wa ngono, mimi kamwe sikuona
kitu chochote tofauti na mwanamke" alisema.
Kwa miaka yote
hiyo 19 wanandoa hao walikuwa wakiishi kwa maisha ya kawaida ya furaha, na Monica
alikuwa kama dada mkubwa wa watoto wake hadi ndoa yao ilipoanza kuingia katika
mkwaruzo hasa pale Monica alipopata ajira.
“Monica alianza
kubadilika sana” alisema Jan
Wakati mwingine
mwanangu mkubwa alikutana na Monica (mama yake wa kambo) kwenye clab za muziki
za usiku akiwa amevalia nguo fupi sana na t-shirt iliyoacha tumbo wazi hadi
kwenye kitovu.
Hata hivyo
fununu zilianza kuzagaa kuwa Monica alikuwa ni mwanume aliyejibadilisha jinsia.
Mwanangu aliweza kunasa mawasiliano yake na wanaume wenzake kwenye komputa yake
na ndipo tulipopata uhakika kwamba Monica niloiyeishi naye kwa miaka 19 hakuwa
mwanamke bali mwanaume aliyefanyiwa opereshini na kuwekewa maumbile ya kike.
Nilipopata uhakika
huu nilikasirika sana. “Nilimsukuma kwenye ukuta wa nyumba yetu kwa hasira sana”
Sasa nimegundua kuwa Hon ambalo ndo jina lake halisi alikuwa sio mwanamke halisi.
Baada ya mzozano mkali Hon alikiri kwamba kweli yeye hakuwa mwanamke kwani
alizaliwa kama mvulana na kwamba ailifanyiwa upasuaji na kubadilishwa kuwa
mwanamke.
Hata hivyo mzozo ule ulipelekewa kupigwa simu
polisi na ndipo kesi ya kutengana naye ikaanza.
Siku yao ya ndoa
Habari hii imetafsiriwa na mdau wa golden blogspot kutoka mtandao wa telegraph
Ukitaka kuisoma kwa Kiingereza bofya hapa:
http://www.telegraph.co.uk/news/worldnews/europe/belgium/9703166/Belgian-discovers-his-wife-used-to-be-a-man-after-19-years.html
No comments:
Post a Comment