Waandamanaji mjini Sidi Bouzid wamemrushia rais wa Tunisia, Moncef Marzouki nyanya na mawe.
Walinzi wa riasi huyo Tunisia, taifa ambalo
mageuzi katika nchi za Kiarabu yalianziawalimuondoa kutoka mahala hapo
na kukatiza mkutano wa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuteuliwa kwake.Mchuuzi mmoja Mohamed Bouazizi, alijiteketeza moto mjini Sidi Bouzid, na kupelekea maandamano makubwa yaliyosaababisha kuondolewa madarakani kwa serikali iliyopita.
Serikali ya sasa imekabiliwa na maandamano kutoka kwa raia ambao wanahisi kuwa serikali ya sasa haifanyi lolote kuimarisha hali ya maisha yao.
Waandamanaji hao walivamia eneo ambalo rais Marzouki, alikuwa amelihutubia umati wa watu wapatao elfu tano.
Raia wataka serikali kuimarisha hali ya maisha
Waandamanaji hao waliimba nyimbo zinazosema ''raia wanataka kuanguka na serikali'', moja ya kauli mbiu iliyotumiwa kuangusha serikali ya rais wa zamani wa nchi hiyo Zine al-Abidine Ben Ali, Januari 2011.
Machafuko hayo kisha yakasambaa hadi Misri, Libya na mataifa mengine ya Kiarabu.
Katika hotuba yake, rais Marzouki alihaidi mageuzi ya kiuchumi katika kipindi cha miezi sita ijayo kwa raia hao wa Sidi Bouzidi, moja ya miji masikini zaidi nchini humo.
Source: BBC News
No comments:
Post a Comment