
Waziri
Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi
cheti Mzee Chrisant Mzindakaya Mwenyekiti wa Kampuni ya kuzalisha
Nyama ya Mkoani Rukwa kwa Mchango wake katika kupambana na Malaria
Nchini. (Picha staffphotographer).
Wadau
makampuni na taasisi mbalimbali wanaopambana na ugonjwa wa malaria
nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda
baada ya uzinduzi wa ‘Malaria Safe Campaign’.
Wizara
ya afya na ustawi wa jamii kwa kushirikiana na kampeni ya tuungane
kutokomeza malaria ,Unite against malaria (UAM) inaendeleza mapambano
dhidi ya malaria kwa kuanzisha mpango wa kuzishirikisha kampuni na
taasisi binafsi za hapa nchini ili ziwe mstari wa mbele katika mapambano
dhidi ya malaria kwa kuwakinga na kuwapatia tiba sahihi wafanyakazi
wao, mpango huu unajulikana kama malaria safe program.
Mpango
wa safe malaria umezinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania , mh Mzingo Pinda.tarehe 29,Nov,2012 katika ukumbi wa kibo
,Hyatt Regency –Kilimanjaro hoteli
Malengo ya mpango
-Kushirikisha
makampuni binafsi katika mapambano dhidi ya malaria kwa kuhakikisha
kuwa wafanyakazi wao pamoja na familia zao wanajikinga na malaria na
kupata tiba sahihi ya malaria pale wanapougua.
-Kutoa elimu ya kujikinga na malaria kwa wafanyakzai na familia zao kwa kuhimiza matumizi ya vyandarua vyenye viwatilifu.
-Kuwa
mawakala wa mapambano dhidi ya malaria kwa kuchngia katika uhamasishaji
wa upatikanaji wa rasilimali ili kuendeleza mapambano dhidi ya malaria
nchini.
Mpango
huu pia unalenga katika kuchangia maeneo yenye mapungufu ya rasilimali
fedha, katika kutoa kinga na tiba sahihi ya malaria nchini, ili kuweza
kufikia malengo yaliyowekwa na serikali katika kuboresha afya za
watanzania na hivyo kuchangia katika kuimmarisha utoaji huduma za afya
kwa mapambano dhidi ya malaria nchini.
Makampuni
binafsi ambayo yamejiunga na mpango huu wa malaria safe na yapo tayari
kuelekeza nguvu zao katika apambano dhidi ya malaria hapa nchini
yatatunukiwa cheti cha utambuzi (certificate of recognition) ambacho
kitatolewa na mgeni rasmi wa uzinduzi.
Ukubwa
wa tatizo la ugonjwa wa malaria unatammbulika dunia nzima, hapa nchini
kutokana na takwimu ,inakadiriwa takribani watu milioni 10 hadi milioni
12 wanaugua malaria kila mwaka, na malaria husababisha vifo vya watu
kati ya 100,000 hadi 300,000 kila mwaka. Aidha zaidi ya asilimia 40 ya
wagonjwa wanaohudhuria katika vituo vya kutolea huduma za afya
wanasumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
Katika
kudhibiti ugonjwa wa malaria serikali kupitia wizara ya afya na ustawi
wa jamii inatekeleza mikakati inayolenga katika kuboresha kinga na tiba
sahihi ya ugonjwa wa malaria.
Kwa
upande wa kinga, umiliki (ownership) wa vyandarua vyenye viwatilifu
vya muda mrefu ueongezeka katika miaka mitano iliyopita , na kufikia
asilimia 91 na hii imetokana na kampeni mbalibali za ugawaji wa
vyandarua zilizofanyika hapa nchini.
Kampeni
hizo ni pamoja na ugawaji vyandarua kwa watoto wenye umri chini ya
miaka mitano,upatikanaji wa vyandarua kwa wanamama wajawazito kupitia
mpango wa hati punguzo na ugawaji wavyandarua kwa wananchi wote kwa
ujumla sehemu za malazi katika kaya kupitia kampeni ya ugawaji wa
vyandarua katika sehemu za malazi.
Njia
nyingine za kinga ni upuliziaji wa dawa ukoko katika kuta ndani ya
nyumba (indoor residual spraying)IRS , zoezi ambalo linaendelea
katikia mikoa mitatu ya kanda ya ziwa;kagera,mwanza na mara, na mradi wa
kuangamiza viluwiluwi vya mbu katika mazalia(Larviciding) zoezi ambalo
linatekelezwa katikia mkoa wa dar es salaam.
Kadharika
tiba ya malaria ,imeboreshwa kwa kuhakikisha kuwa tiba sahihi ya
malaria kwa kutumia dawa mseto inapatikana katika vituo vya kutolea
huduma za afya na sekta binafsi kwa bei ya punguzo .kwa upande wa
upimaji wa vimelea vya malaria,sambamba na matumizi ya hadubini
(microscope) pia matumizi ya kipimo cha utambuzi wa vimelea vya
malaria kwa haraka (malaria rapid diagnosis tests-Mrdts, yanaendelea
baada ya kukamilika kwa mafunzo kwa watoa huduma nchi nzima.
Mafanikio
yanaonekana, kutokana na mikakati iliyoanishwa hapo juu ,takwimu za
utafiti wa vishiria vya malaria na virusi vya ukimwi )Tanzania HIV/AIDS
na malaria indicators survey 2011/2012 zilizotolew hivi karibuni
zinaonesha kuwa maambukizi /uwepo wa vimelea vya malaria kwa watoto
chini ya miaka mitatno umepungua kwa asilimia 45 kutoka asilimia 18 kwa
mwaka 2007/2008 kufikia asilimia 10 kwa mwaka 2011/2012.
Hata
hivyo bado zipo changamoto mbalimbali katika mapambano dhidi ya malaria
hapa nchini ,kutokana na takwimu kutoka katika vituo vya huduma,
malaria bado inaongoza katika matukio ya ugonjwa na vifo.pia malaria
inaleta changamoto katika uzalishaji mali na hivyo kuchangia katika
athari za kiuchui na hatimmaye maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Kwa
kushirikisha kampuni binafsi katika mapambano dhidi ya malaria
,tunaamini itasaidia katika kupunguza athari za malaria kwa jamii na kwa
nchi ,kujiunga na mpoango wa malaria safe,makampuni yatatekeleza mambo
manne muhimu.
1. Elimu;kukubali kueliisha wafanyakazi wake juu ya athari na tiba sahihi ya malaria
2. Kinga ;kuwakinga wafanyakazi wake kwa kuhakikisha wanatumia vyandarua vyenye viwatilifu vya muda mrefu.
3. Muonekano; kuweka ujumbe wa malaria katika huduma wanazotoa/wanazozalisha.
4. Utetezi; kukubali kuwa balozi wa kutetea mapambano dhidi ya malaria na kuhamasisha makampuni mengine kujiunga na mpangfo huo.
Serikali
ya Tanzania inawajibu wa kiuhakikisha kwamba mikakati ya kupambana na
malaria inakuwa endelevu kwa kushirikiana na sekta binafsi pamoja na
wadau wengine wa malaria.
Mpango
huu wa malaria safe,utakuwa ni moja kati ya chachu za kuhamasisha
utekelezaji wa mikakati ya kudhibiti malaria na hivyo kuchangia kupungua
kwa ugonjwa wa malaria na hatimaye kuitokomeza kabisa .
Kwa pamoja tuungane kuitokomeza malaria
Malaria Haikubaliki- Tushirikiane kuitokomeza
kilakukicha tararira
ReplyDelete