ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, December 3, 2012

Enneagram (zijue aina tisa za tabia za watu)

 

Enneagram ni elimu ya kujua aina mbali mbali za watu na tabia zao. Hili ni somo muhimu sana kwani katika maisha yetu ya kila siku tunajikuta tunaishi miongoni mwa watu wengi na kila mmoja akiwa na tabia yake. Unapojua aina ya tabia ya mwenzako (personality) inakupa maarifa ya kujua namna ya kuishi naye. Kwa mfano kama bosi wako kazini ni namba 6 na wewe mfanyakazi wake ni namba 1 pengine mtakuwa mnaingia katika  mzozo kila siku kwa sababu ya typology yenu kuwa tofauti. Hivyo Namba moja ambaye ni mwajiriwa, ili aweze kuishi na namba 6 ambaye ni bosi ni lazima apate nguvu kwa typology mwingine ambaye ana aina tofauti ya tabia.  
Hivyo kama lilivyo jedwali hapo juu, kuna aina tisa za watu/tabia.
1. mzuzi/mkamilifu
2. Msaidizi/mtoaji
3. achiever (sijapata kiswahili sahihi, natafuta bado)
4. kibinafsi/mbinafsi/..
5. Mpelelezi/mwangaliaji/msimamiaji
6. waaminifu/mwenye mashaka na kila kitu
7. Enthuiast/mwotaji
8. Challenger/kiongozi/kiherehere
9. msuluhishi 


Fuatilia makala hii ambapo kila siku kwa siku tisa nitakua nakupa maelezo ya kila aina ya tabia na siku ya kumi nitakupa mjumuisho wa tabia zote pamoja na kujua ni tabia ipi itaendana na wewe kutokana na aina yako ya tabia. Hii ni muhimu sana kwa kila mtu. Watu wanaoishi kwa makundi katika jamii kama vyuoni, mashuleni, makambini, makanisani, makazili. Na zaidi mno kwa wale wanaotarajia kuoana. Ni vizuri mno kujua mwezi wako unayetaka kufunga naye ndoa ni tabia ipi na wewe ni tabia ipi. Mkioana wenye tabia kinzani sana basi hiyo ndoa itaota mbawa siku chache sana. Na kama umeshaoa au kuolewa na mtu ambaye baadaye umegungua tabia zenu haziendani basi ni nafasi pekee ya kuweza kujua ni wapi pa kushika kwani utakuwa na uwezo wa kuelewa tabia yake kitaalamu na ya kwako yaani utaelewa uwezo wake na udhaifu wake kitabia (point of strenght and point of weaknes) then mtaweza kuishi vizuri
Na mdau wako Richard Bahati

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...