ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Saturday, December 29, 2012

Taswira Za Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad Alivyotua Tanga na Kuhutubia Mkutano wa Hadhara

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bibi Chiku Galawa akimkaribisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katika Mkoa huo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimia na vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi wa Mkoa wa Tanga, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimia na wananchi mbali mbali waliojitokeza kumpokea wakati walipowasili katika uwanja wa ndege wa Tanga kwa ziara ya siku mbili.
   Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
  Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha kadi za ADC zilizorejeshwa na baadhi ya wafuasi wa chama hicho na kujiunga na CUF katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...