ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Saturday, December 29, 2012

Watu 8 wafariki katika eneo ya Kerio Magharibi mwa Kenya

Familia zilizoathiriwa
Familia zilizoathiriwa kwa mujibu wa Gazeti la Standard Nchini Kenya wakipekuwa mali yao baada ya maporomoko hayo ya Ardhi
 

  
 
Picha mbali mbali zikionyesha madhara yaliyosababishwa na mvua na maporomoko ya ardhi huko Kerio Magharibi mwa Kenya

Watu wanane wamekufa baada ya nyumba kadha kufukiwa na maporomoko ya ardhi katika eneo la bonde la Kerio, magharibi mwa Kenya, jana usiku.
Maporomoko ya ardhi yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha katika bonde hilo. Eneo la Kerio pia limekumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayonyesha.
Chama cha Msalaba Mwekundu cha Kenya kinasaidia jitihada za uokoaji na kutoa taarifa kwamba miili  ya watu wanane imeonekana na watu wengine watano waliokolewa mapema leo.
Watu wengi hawana makaazi kutokana na nyumba zao kusombwa na maji au kufukiwa na maporomoko ya ardhi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...