Waziri
wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akizungumza na
waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali juu ya suala zima la kuuingia
katika mfumo wa Digitali katika ukumbi wa habari maelezo kikwajuni mjini
Zanzibar.
Mwandishi
wa habari Bw.Salum Vuai akiuliza suali kwa Waziri hayupo pichani juu ya
upatikanaji wa vinga`muzi katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa
habari maelezo mjini Zanzibar.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akijibu maswali
ya waandishi wa habari hawapo pichani kulia ni Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Bihindi Khamisi Hamadi.
Jengo
linalotarajiwa kufungwa vifaa vya mitambo ya Digitali lililopo Rahaleo
mjini Zanzibar.(Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imesema matangazo ya mfumo wa Analogia yatazimwa
rasmi katika Mikoa yote ya Zanzibar ifikapo Februari 28 mwakani ili
kupisha mfumo mpya wa matangazo kwa njia ya Dijitali.
Waziri wa
habari, utamaduni, utalii, na Michezo Said Ali Mbarouk ameyasema hayo
alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari
maelezo kikwajuni mjini Zanzibar kuhusiana na matayarisho ya kuhamia
katika mfumo mpya wa matangazo ya Dijitali.
Amesema
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kamisheni ya Utangazaji
Zanzibar (ZBC) zimeshauriana na kukubaliana kuwa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania iingie katika mfumo mpya wa Dijitali kwa awamu ambapo kwa zoni
ya ZanzĂbar imekubaliwa kuwa February 28 2013 ndio iwe mwisho rasmi wa
matangazo ya Analogia
Waziri
Mbarouk amesema Wizara yake haitozima mitambo ya matangazo ya Analogi
ifikapo Disemba 31 bali itakachofanya ni kutangaza kwa pamoja matangazo
ya Analogi na Digitali kwa mfumo unaojulikana kitaalamu kama SIMU L CAST
hadi itakapofika muda rasmi wa kuhama mfumo wa Analogy.
Akizungumzia
matayarisho ambayo yamefanywa na Wizara yake katika kuukabili mfumo
mpya wa Matangazo ya Dijitali Waziri Mbarouk amesema tayari wamejenga
kituo cha usambazaji ishara(signals) katika eneo la Rahaleo
kitakachokuwa na kazi ya kupokea na kusambaza ishara na mitambo ya
uendeshaji.
Aidha Wizara
imetayarisha maeneo matatu Unguja ambayo ni Kizimkazi,Masingini na
Nungwi ambapo kwa upande wa Pemba ni Kichunjuu,Mkanjuni na Konde kwa
ajili ya kurushia matangazo ya Dijitali.
Matayarisho
mengine ni pamoja na kuandaa utaratibu mzuri wa upatikanaji wa
Ving’amuzi na maudhui kwa bei nafuu ambapo amesema vitaanza kuuzwa
mwishoni mwa mwezi wa Januari mwakani.
Amefahamisha
kuwa bei ya Ving’amuzi hivyo itakuwa rahisi kuliko vingamuzi vingine
ambapo mwananchi atatakiwa kukinunua kwa Sh l50,000 na kukilipia sh
l8,000 kwa mwezi ili kupata huduma ya matangazo hayo.
Amevielezea
Ving’amuzi hivyo ambavyo vitakuwa na huduma mbali mbali ikiwemo Mtandao,
Video on demand, programme guide, exclusive service yaani mawasiliano
ya makundi maalum ambapo pia jumla ya Chaneli 36 za ndani na nje ya nchi
zitapatikana kwa uhakika.
Waziri
Mbarouk amesema uzinduzi wa mitambo na matangazo ya Dijitali unatarajiwa
kufanyika wakati wa sherehe za Mapinduzi Januari 8 mwakani katika
maeneo ya Rahaleo mjini Zanzibar.
Mabadiliko
ya Mfumo wa matangazo kutoka Analogia kwenda Dijitali yamekuja kufuatia
agizo lililotolewa na Shirikisho la Mawasiliano la Afrika Mashariki EACO
kuwa Nchi wanachama wa Shirikisho hilo ziwe zimehamia katika mfumo mpya
wa Dijitali ifikapo mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment