
Zaidi
ya abiria 25 waliokuwa wakisafiri na ndege ya Shirika la ndege nchini
ATCL kutoka Kigoma kuelekea Dar es Salaam wamenusurika kifo kutokana na
ndege waliyokuwa wakisafiria kupata hitilafu ikiwa angani jambo
lililomlazimu rubani wa ndege hiyo kufanya jitihada na kuirudisha
kiwanjani.
Hali
hiyo imetokana na moja ya vioo vya mbele vya ndege hiyo kupasuaka na
hivyo kuruhusu upepo mkali kuingia ndani na hivyo kuwafanya marubani wa
ndege hiyo kufanya kazi ya ziada kuhakikisha ndege hiyo inatua salama.
Ndege
hiyo ilikuwa ikifanya safari yake ya kwanza mkoani humo ikiwa ni miezi
10 baada ya ndege nyingine ya shirika hilo kuanguka na kuharibika mkoani
Kigoma.
Baadhi
ya abiria waliokuwemo kwennye ndege hiyo, Athumani Batumwa na Fred
Mbassa wamesema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 50, ilipata
itilafu ya kioo cha mbele kiasi cha dakika 30 baada ya kuruka kutoka
uwanja wa ndege wa Kigoma.
Kaimu
meneja wa shirila la ATCL, Kepteni Milton Lazaro amekiri kutokea kwa
hitilafu hiyo na amewaondoa hofu wasafiri juu ta tatizo hilo nakwamba ni
sehemu ya matatizo yanayoweza kutokea kwa ndege yoyote.
via blogu ya Lukwangule
No comments:
Post a Comment